Na Mapuli Kitina Misalaba
Tamasha la
19 la Himaya ya Jigoku (Masela), Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, likiongozwa na
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia
Sangalali, limehamasisha amani, maadili na uendelezaji wa mila na desturi za
Kitanzania.
Akizungumza
katika tamasha hilo, Chifu Sangalali amesema matamasha hayo yataendelea
kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuendeleza mila na tamaduni za Kitanzania,
kutoa burudani na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani na maadili.
Amesema
matamasha hayo pia ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kupunguza uhalifu
katika jamii, huku akiwataka wananchi kuendelea kuiheshimu Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na kuweka amani mbele.
“Tutaendelea
kuwaletea matamasha haya kila mwaka yakiambatana na ngoma za asili ili
tuburudike. Hii ni sehemu ya kupunguza uhalifu. Tuendelee kuiheshimu Serikali
yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuendelee kuiweka amani mbele na
maadili tuyafuate ili tuweze kuishi kwa amani,” amesema Chifu Sangalali.
Katika
tamasha hilo, Chifu Sangalali pia ametoa ujumbe wa Benki Kuu ya Tanzania kwa
wananchi kuhusu utunzaji wa noti, akiwataka kutokuzichana, kuzitoboa wala
kuziandikia kwa kuwa fedha hizo hutumiwa na watu mbalimbali.
Aidha,
amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa mvua za El Niño,
ikiwemo kutunza chakula na kuondoka katika maeneo hatarishi endapo kutatokea
mvua kubwa na mafuriko.
Chifu
Sangalali pia ametoa wito kwa wanafunzi, hususan wasichana, kuzingatia elimu na
kutokukimbilia ndoa kabla ya kukamilisha masomo yao.
Kwa upande
wake, mgeni rasmi katika tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Vicent
Anney, amempongeza Chifu Antonia Sangalali kwa kuendeleza tamasha hilo kila
mwaka, akisema ni sehemu muhimu ya kuhifadhi historia ya machifu nchini
Tanzania.
Amehimiza
wananchi kuendelea kulinda amani, mshikamano, mila na desturi za Kitanzania,
akisisitiza kuwa taifa haliwezi kuwa bora bila kuheshimu na kuhifadhi utamaduni
wake.
Mkuu huyo wa
Wilaya amewataka pia vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na
mshikamano katika jamii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.
Baadhi ya
wakazi wa Himaya ya Jigoku wamempongeza Chifu Antonia Sangalali kwa kuendelea
kuandaa tamasha hilo kila mwaka, wakisema limekuwa likiwapa fursa ya kukutana,
kuburudika pamoja na kupata elimu na ujumbe mbalimbali kuhusu maisha ya jamii.
Tamasha hilo
pia limewakutanisha ndugu wa utemi wa Chifu Sangalali kutoka maeneo mbalimbali,
ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma na Kagera, pamoja na wageni kutoka nchini Uganda.
Burudani
mbalimbali za ngoma za asili zimetawala katika tamasha hilo, huku msanii
maarufu wa ngoma za asili, Shule ya Ng’ombe, akiongoza kutoa burudani na
kuifanya siku kuwa ya kipekee kwa
washiriki.
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia Sangalali ni mmoja wa waazilishi wa matamasha hayo yanayowakutanisha machifu na jamii, hivyo ametumia nafasi hiyo kuhimiza kuendelea kuyafanya kwa kuwa ni sehemu ya kuhifadhi historia, mila na tamaduni za Kitanzania.
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia Sangalali, akizungumza wakati wa Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku, Maswa mkoani Simiyu.
Chifu Antonia Sangalali akitoa ujumbe mbalimbali kwa wananchi wakati wa Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania, Chifu Antonia Sangalali, akizungumza katika tamasha hilo lililolenga kuendeleza mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Vicent Anney, akizungumza wakati wa Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Vicent Anney, akimpongeza Chifu Antonia Sangalali kwa kuendeleza Tamasha la Utamaduni la Himaya ya Jigoku kila mwaka.
Chifu Antonia Sangalali na Dkt. Vicent Anney wakifuatilia shughuli mbalimbali katika Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Ndugu wa utemi wa Chifu Antonia Sangalali kutoka maeneo mbalimbali wakishiriki Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Ngoma za asili zikitumbuiza katika Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku, Maswa mkoani Simiyu.
Ngoma za asili zikitumbuiza katika Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku, Maswa mkoani Simiyu.
Burudani za ngoma za asili zikiongozwa na msanii Shule ya Ng’ombe zikinogesha Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Msanii Shule ya Ng’ombe akipongeza na chifu Antonia Sangalali kwenye Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Msanii Shule ya Ng’ombe akipewa zawadi ya fedha na chifu Antonia Sangalali kwenye Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Msanii Shule ya Ng’ombe akisalimiana na wanaukoo wa chifu Sangalali kwenye Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Burudani za ngoma za asili zikiongozwa na msanii Shule ya Ng’ombe zikinogesha Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Burudani za ngoma za asili zikiongozwa na msanii Shule ya Ng’ombe zikinogesha Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Ndugu wa utemi wa Chifu Antonia Sangalali kutoka maeneo mbalimbali wakishiriki Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku.
Ngoma za asili zikitumbuiza katika Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya ya Jigoku, Maswa mkoani Simiyu.
Awali wazee wa Himaya ya Jigoku wakichuana katika mchezo wa bao kabla ya kuanza kwa shughuli za Tamasha la Utamaduni la 19 la Himaya hiyo.

Makaburi ya baadhi ya ndugu wa ukoo wa Himaya ya Jigoku, yakihifadhi historia na kumbukumbu ya vizazi vilivyotangulia.
Makaburi ya baadhi ya ndugu wa ukoo wa Himaya ya Jigoku, yakihifadhi historia na kumbukumbu ya vizazi vilivyotangulia.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment