Chuo Cha Uhasibu Arusha(IAA) kimejinyakulia tuzo ya mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma zisizo za kibiashara zinazofanya vizuri katika usimamizi na matumizi bora ya fedha(Best Financial Management Perfomance -Non-Commercial Entities).
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la upngozi IAA,Dkt Mwamini Tulli na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Deogratias Ndejembi katika kikao cha wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi za umma(CEOs Forum) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mkuu wa chuo hicho,Dr Eliaman Sedoyeka amesema kwamba mara baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuzitaka taasisi za umma zijipambanie katika makusanyo na matumizi Chuo chao kilianza kufanya jitihada za dhati kuhakikisha wanatimiza azma hiyo na sasa wanajivunia kwa kupiga hatua.
Dkt Sedoyeka amesema kwamba wamenza kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais,Dkt Ndejembi aliyoyatoa katika mkutano huo kuhusu kuwawezesha vijana kwa kuwapatia ujuzi ,weledi na uelewa wa pamoja katika masuala ya biashara ili kuwafungulia milango ya kuajiri na kujiajiri.
Amesema kwamba tayari chuo chao kimeanza kuboresha mitaala inayoendana na soko la ajira katika masomo ya fedha ,utawala ,bima ,utalii ,uanagenzi posta na vifurushi kama njia mojawapo ya kuwaandaa vijana kuingia katika soko la ushindani wa ajira na biashara kwa ujumla.
Dkt Sedoyeka amesisitiza ya kwamba mpaka sasa chuo chao kimeandaa watalaamu ambao wanawaandaa vijana kuanzisha mawazo ya kibiashara na mpaka sasa tayari wamefanikiwa kuanzisha makampuni 20 na yake yasiyo rasmi zaidi ya 50.




Post a Comment