Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Fredy Liundi amesema takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zinaonesha kuwa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu mauzo ya madini nchini yamefikia takribani shilingi Trilioni 7.78.
Akizungumza leo Septemba 27, 2026, katika hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo unaofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, Liundi amesema mauzo hayo yameongezeka ikilinganishwa na mauzo yaliyofanyika kwa mwaka mzima wa 2025, ambapo yalikuwa takribani Trilioni 11.7 ukilinganisha na Trilioni 7.78 zilizopatikana takribani ndani ya nusu mwaka.
Katika hatua nyingine, Liundi amesema mwaka 2021, wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani, mauzo ya madini nchini yalikuwa takribani Trilioni 7.2 kwa mwaka jambo ambalo amedai ongezeko la mauzo kwa mwaka huu (hadi kufikia Julai, 2026), ni ishara tosha ya matunda ya jitihada zinazofanywa na Serikali.
Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa na wafanyabiashara wa madini nchini jambo ambalo amesema linaendelea kuongeza uwezo wa Serikali kukusanya mapato yake kupitia Sekta ya Madini.
Aidha Kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2025/2026, Sekta ya Madini imeelezwa kuchangia asilimia 10 ya Pato la Taifa, huku zaidi ya asilimia 56 ya fedha za kigeni zinazoingia nchini zikitokana na mauzo ya madini.
Kwa upande wa wachimbaji wadogo imeelezwa kuwa wamechangia asilimia 40 ya mapato ya Serikali yatokanayo na shughuli zao za uchimbaji madini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, leo Septemba 27, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa maonesho ya tisa ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Dkt. Kiruswa amesema kuwa Serikali inapanga kuongeza mchango wa sekta hiyo kwa kupanua wigo katika masuala ya utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji na uongezaji thamani wa madini pamoja na utoaji huduma mbalimbali katika maeneo yenye shughuli za madini.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment