Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, amemteua tena rasmi Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hatua inayofungua ukurasa mpya katika kukamilisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, uteuzi huo umeanza kutekelezwa mara moja huku Othman akitarajiwa kuapishwa rasmi katika hafla itakayofanyika Ikulu Zanzibar.
Hatua hii inafuatia mchakato wa ndani wa chama cha ACT Wazalendo kumteua kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, kufuatia makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa kati ya CCM na ACT Wazalendo mnamo mwezi Julai mwaka huu kwa lengo la kuimarisha siasa za maridhiano visiwani humo.
Uteuzi huu unakamilisha mfululizo wa hatua muhimu zilizochukuliwa na Dk Mwinyi, zikiwemo uteuzi wa Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia nafasi za uteuzi wa rais, ambao tayari wameshaapishwa na kuanza majukumu yao.
Baada ya kuapishwa kwa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, mamlaka zinatazamiwa kukamilisha uteuzi wa baraza jipya la mawaziri ili kujaza nafasi nne zilizo wazi ikiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, pamoja na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, hatua ambayo imepongezwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini wakisema italeta mshikamano mkubwa na kuleta tija ya kimaendeleo kwa Wazanzibari wote
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment