Tanzania imebainisha maeneo muhimu ambayo Afrika inapaswa kuyapa kipaumbele katika kujiandaa na matumizi ya teknolojia zinazolinda taarifa katika miundombinu ya umma ya kidijitali, ikisisitiza umuhimu wa kujenga misingi imara ya kisheria, kitaasisi, kiteknolojia na kiusalama kabla ya teknolojia hiyo kutumika kwa upana.
Mtazamo huo umewasilishwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, wakati akifungua mjadala uliohusu Mifumo na Mustakabali wa Usalama wa Taarifa, Maamuzi ya Kitaifa na Mifumo ya Ulinzi kwa Miundombinu ya Umma ya Kidijitali kwa Kizazi Kijacho uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), jijini New York, Marekani.
Akizungumzia fursa kwa Afrika, Waziri Kairuki amesema teknolojia ya usalama wa taarifa inaweza kupanua wigo wa matumizi ya miundombinu ya kidigitali ya umma kutoka katika mifumo ya utambulisho wa kidijitali, malipo na ubadilishanaji wa data, hadi kuwezesha uwakilishi wa kidijitali wa haki na mali mbalimbali, ikiwemo ardhi, hati fungani, madai ya malipo na mazao yaliyohifadhiwa.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa teknolojia ya usalama wa taarifa haiwezi kuchukua nafasi ya mamlaka halali za usajili wa haki na mali. Badala yake, inapaswa kuwakilisha haki au mali inayotambuliwa na sheria na kuunganishwa na rekodi rasmi na mifumo halali ya usajili.
Ameongeza kuwa msingi huo ni muhimu katika kulinda uhuru wa nchi katika kufanya maamuzi ya kiteknolojia, kuzuia utegemezi wa mfumo au mtoa huduma mmoja, na kuhakikisha mifumo ya kidijitali inaweza kuunganishwa na kubadilika kadri teknolojia na mahitaji ya wananchi yanavyoendelea kukua.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment