
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari Ngokolo, Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Jackline Isaro, akizungumza wakati wa sherehe hiyo na kutoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na wazazi katika kutatua changamoto za shule.
Diwani wa Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, Mhe.
Jackline Isaro, ameahidi kuendelea kushirikiana na jamii katika kutatua
changamoto zinazoikabili shule ya Sekondari ya Ngokolo, ikiwemo ukarabati wa
madarasa na ujenzi wa uzio wa shule hiyo.
Akizungumza katika mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari
Ngokolo, Mhe. Isaro amesema kuna uwezekano wa shule hiyo kupata madarasa mapya
kutoka Serikalini ifikapo mwezi Desemba, huku akiwahimiza wananchi kutokuwa na
hofu kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto za miundombinu.
“Mwezi Desemba tunaweza kupata madarasa mapya kutoka
kwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Niwatoe hofu kupitia risala hii.
Naomba niseme madarasa hayo tutayakarabati,” amesema Isaro.
Aidha, Diwani huyo ameahidi kuchangia mifuko 15 ya
saruji ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusaidia
kuboresha mazingira ya shule.
Mhe. Isaro pia amesema ataendelea kushirikiana na
wananchi katika kipindi cha miaka mitano ambacho wamempa dhamana ya kuwaongoza
katika Kata ya Ngokolo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo, Mwl.
James Msimba awali akisoma taarifa ya shule katika mahafali hayo, ameeleza
baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Miongoni mwa changamoto hizo ni uchakavu wa vyumba
saba vya madarasa, upungufu wa matundu 22 ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na
kukosekana kwa uzio wa kudumu katika eneo la shule.
Mkuu huyo wa shule amewasihi wahitimu kujitambua, kuwa
na nidhamu na kutumia elimu waliyopata kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.
Betha Deus wakati akisoma risala ya wahitimu katika
mahafali hayo kuwa wanafunzi hao wamejiandaa kufanya vizuri katika mtihani wao
wa kuhitimu na kwamba wataendelea kutumia nidhamu na elimu waliyopata kwa
manufaa yao na jamii kwa ujumla .
Jumla ya wahitimu 364 katika shule ya sekondari Ngokolo wamesherehekea siku yao ya kuhitimu kidato cha nne 2026.
Mhe. Jackline Isaro, Diwani wa Kata ya Ngokolo, akitoa salamu zake katika Mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari Ngokolo.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari Ngokolo, Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Jackline Isaro, akizungumza katika hafla hiyo.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment