Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Daudi Silanga, amewataka wakazi wa jimbo la Itilima kutumia kipindi hiki kulima mapema ili kujipatia mazao ya kutosha kutokana na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kuanza mapema mwaka huu.Akizungumza katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika vijiji vya Mwaumishenu,Mwamunemha,Isagara,Kinang'weli,Bukingwamizi,Mwamunhu,Isakang'hwale na kijiji cha Inalo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutoa mrejesho wa hatua za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni Mhe. Njalu amesema ni muhimu kwa wakulima kuanza maandalizi ya kulima mapema ili kuepuka athari zitakazoweza kusababishwa na mvua nyingi.Pia ameeleza jinsi Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoendelea kuboresha huduma na kutekeleza miradi mbalimbali akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kwa ngazi zote ili kuhakikisha miradi na maagizo ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment