Uongozi mpya wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania
(Red Cross) Mkoa wa Shinyanga umefanya kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga, Pili Mnyema, kwa lengo la kujitambulisha rasmi pamoja na kuimarisha
ushirikiano kati ya shirika hilo na Serikali katika kutoa huduma za kibinadamu
kwa wananchi.
Kikao hicho pia kimejikita katika kujadili namna ya
kuimarisha ushirikiano katika masuala ya maafa, majanga, uokoaji, huduma za
dharura na utoaji wa misaada kwa wananchi pindi yanapotokea majanga mbalimbali
katika Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Red
Cross Mkoa wa Shinyanga, Hatibu Mgeja, amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa, Pili
Mnyema, kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kupewa jukumu la kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Mgeja amemkaribisha Katibu Tawala huyo mkoani
Shinyanga na kumhakikishia kuwa uongozi mpya wa Red Cross uko tayari kutoa
ushirikiano wa karibu kwa Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma
muhimu, hususani wakati wa majanga na changamoto zinazohitaji mwitikio wa
haraka.
Amesema Red Cross ina nafasi muhimu katika kusaidia
jamii wakati wa majanga, hivyo ushirikiano na Serikali ni jambo la msingi
katika kuhakikisha maandalizi na mwitikio wa majanga unakuwa wa haraka na wenye
ufanisi.
“Tunampongeza Katibu Tawala wa Mkoa kwa
kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Rais na tunamkaribisha rasmi Mkoani
Shinyanga. Sisi kama Red Cross tupo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote
katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga,” amesema
Mgeja.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga,
Pili Mnyema, amewashukuru viongozi wa Red Cross kwa kufika ofisini kwake katika
siku ya kwanza akiwa katika ofisi yake kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Mnyema amesema Serikali iko tayari kushirikiana na Red
Cross katika utekelezaji wa majukumu yake, akisisitiza umuhimu wa kuwa na
maandalizi ya pamoja katika kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza.
Amesema ushirikiano huo ni muhimu zaidi katika kipindi
ambacho kuna tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua kubwa zinazoweza kusababisha
changamoto mbalimbali ikiwemo mafuriko, uharibifu wa miundombinu na kuathiri
maisha ya wananchi.
“Tunawashukuru wana-Red Cross kwa kuja
kututembelea siku ya kwanza nikiwa ofisini kama Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga. Tutashirikiana nanyi kikamilifu, hasa katika kipindi hiki ambacho
kuna tahadhari ya ujio wa mvua za El Nino,” amesema Mnyema.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na
wadau mbalimbali katika kuhakikisha jamii inaelimishwa, inaandaliwa na
inachukua tahadhari mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na
majanga.
Ushirikiano kati ya Serikali na Red Cross unatarajiwa
pia kusaidia katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira,
tahadhari dhidi ya majanga, maandalizi ya kaya na namna ya kuchukua hatua za
haraka wakati wa dharura.
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Shinyanga, Hatibu Mgeja, akizungumza kwenye kikao hicho ambapo amempongeza Katibu Tawala Pili Mnyema kwa kuendelea kuaminiwa na Rais na kumuahidi ushirikiano katika kuwatumikia wananchi.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Pili Mnyema, amesema Serikali iko tayari kushirikiana na Red Cross katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wa majanga.
Uongozi mpya wa Red Cross Mkoa wa Shinyanga umekutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Pili Mnyema, kwa lengo la kujitambulisha na kuimarisha ushirikiano katika huduma za kibinadamu na kukabiliana na majanga.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment