Na Mwandishi Wetu, DODOMAKanda Namba Tatu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya zoezi la usafi katika maeneo ya Kizota Relini na Mkonongo, Kata ya Nkuhungu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño.Zoezi hilo lilihusisha ufunguaji na usafishaji wa mitaro, uondoaji wa taka pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya kupitisha maji, hatua zinazolenga kupunguza hatari ya maji kujaa katika maeneo ya makazi na biashara.Kaimu Meneja wa Kanda Namba Tatu, Vestina Manota, aliwashukuru watumishi na wananchi kwa kushiriki katika zoezi hilo, akisema usafi wa mazingira ni muhimu katika maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za El Niño.“Tunawahimiza wananchi kuendelea kufanya usafi kila siku na kuondoa taka kwenye mitaro ili kuhakikisha maji yanapata njia ya kupita kwa urahisi,” alisema Manota.Diwani wa Kata ya Nkuhungu, Julius Ezekiel, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari mapema kwa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mwenendo wa mvua, pamoja na kuendelea kufanya usafi wa maeneo yao kila siku.Naye Afisa Afya, Consolata Urio, alisema usafi husaidia kuzuia maji kutuama, kuzaliana kwa mbu na kuenea kwa magonjwa, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha maeneo yao ya makazi na biashara yanakuwa safi wakati wote.Kwa niaba ya wananchi, Ally Salim, alisema zoezi hilo limeimarisha umoja na mshikamano katika kukabiliana na athari za mvua, huku Halmashauri ikiwasisitiza wananchi kuendelea kufanya usafi kila siku, kutunza mitaro na kuepuka kutupa taka kwenye njia za maji.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment