Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amepongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa mafanikio makubwa katika kuimarisha thamani ya mfuko na kuboresha huduma kwa wanachama na wastaafu, akisema PSSSF ni mfano wa kuigwa katika usimamizi wa rasilimali za wanachama.
Sangu ameyasema hayo alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini mjini Geita, akibainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, thamani ya mfuko imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 7.4 Serikali ilipoingia madarakani hadi kufikia Shilingi trilioni 16.96 hivi sasa. Amesema ongezeko hilo la zaidi ya mara mbili linaonesha uthabiti, uwazi na usimamizi thabiti wa rasilimali za wanachama.
Kuhusu ulipaji wa mafao, Sangu amesema kupitia kaulimbiu ya “Tunalipa Jana”, wastaafu hupata mafao yao mara wanapostaafu, huku pensheni ya kila mwezi ikilipwa kabla ya tarehe 25. Ameongeza kuwa PSSSF inaendelea kushirikiana na waajiri kutoa elimu na kuwaandaa watumishi kabla ya kustaafu, huku akiwataka watumishi kujiandaa mapema ili kurahisisha upatikanaji wa mafao kwa wakati.
Katika eneo la matumizi ya TEHAMA, Sangu amesema PSSSF imeendelea kuwekeza katika mifumo ya kidijitali inayorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu. Miongoni mwa mifumo hiyo ni PSSSF KIDIJITAL, unaomwezesha mstaafu kuhakikiwa kidijitali akiwa popote alipo, hatua inayosaidia kuondoa adha ya kusafiri hadi ofisi za Mfuko kwa ajili ya uhakiki.
Amesema maboresho hayo yanaonesha namna PSSSF inavyoendelea kuimarisha huduma kwa kutumia teknolojia na kuweka mazingira rafiki kwa wastaafu kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati, huku akisisitiza umuhimu wa watumishi kuendelea kupata elimu kuhusu mafao na maandalizi ya kustaafu.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment