Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ameteua wajumbe 10 kuunda Kamati ya Pamoja ya Majadiliano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na chama cha ACT Wazalendo, ikiwa ni hatua ya kuendeleza utekelezaji wa Tamko la Pamoja la Makubaliano kuhusu ajenda za kufanyiwa kazi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mansura Kassim, imeeleza kuwa wajumbe hao wameteuliwa baada ya vyama hivyo viwili kuwasilisha majina ya viongozi waliopendekezwa kuunda kamati hiyo itakayozinduliwa rasmi Ikulu mjini Unguja.
Katika uteuzi huo, Abdi Mahmoud Abdi na Omar Ali Shehe wameteuliwa kuwa wajumbe na Wenyeviti Wenza wa Kamati, huku wajumbe wengine wakiwa ni Dk. Khalid Salum Mohamed, Najma Murtaza Giga, Masoud Ali Mohamed, Mgeni Hassan Juma, Omar Said Shaaban, Fatma Abdulhabib Fereji, Said Ali Mbarouk na Mohamed Nur Mohamed. Aidha, Rais amewateua Mwalim Ali Mwalim na Seif Khamis Mohamed kuwa Makatibu Wenza, huku sekretarieti ikiundwa na Hamid Saleh Mhina, Mohamed Yusuf Nuh, Ali Salim Khamis na Abdalla Mussa Hijja.
Hatua hii inafuatia kusainiwa kwa Tamko la Pamoja la Makubaliano kati ya CCM na ACT Wazalendo mnamo Julai 9, 2026, katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja, lenye lengo la kuendeleza mazungumzo na kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto za kisiasa zilizojitokeza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Wakati wa hafla hiyo, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa vyama hivyo vimefanya jambo la kiungwana linalofundisha staha, utu na kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya kiburi.
Naye Rais wa Zanzibar, Dk. Mwinyi alieleza dhamira ya dhati ya kusimamia mchakato huo akibainisha kuwa wananchi wengi ni waumini wa amani na mshikamano, kauli iliyoungwa mkono na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Masoud Othman Masoud, aliyeeleza kuwa maridhiano hayo yanalenga ujenzi wa Zanzibar yenye utulivu, utawala bora na maendeleo endelevu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment