Madereva wa vyombo vya moto mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kufunga taa za vimulimuli pamoja na ving'ora kwenye magari, pikipiki na bajaji zao pasipo kuwa na sifa na ruhusa kwa mujibu wa sheria.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika Stendi ya Soko kuu Mkoa wa Shinyanga.Sajenti Ndimila amewaeleza madereva hao kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la madereva wa magari ya kawaida, daladala, pikipiki na bajaji wanaotumia vifaa hivyo kiholela kwa madhumuni ya kupenya foleni na kujipatia kipaumbele barabarani.Aidha amewaeleza kwamba tabia hiyo imekuwa ikipunguza heshima ya magari ya dharura na kusababisha wananchi kushindwa kupisha magari ya kuokoa maisha kwa wakati.Pia amewaelimisha kuwa Kwa mujibu wa Kanuni za Usalama Barabarani na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini LATRA, ni kosa kisheria kwa mtu binafsi wa chombo Cha moto kufunga na kutumia ving'ora au taa za vimulimuli bila ruhusa ya mamlaka husika.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment