Tume ya Maendeleo ya Vyama Ushirika imewataka watanzania kuweka akiba kwenye vyama vya ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu waweze kukuza uchumi wao.
Hayo yamebainishwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Mwanza Hilda Boniface alipokuwa akizungumza kwenye maonesho ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.
Aliwataka wananchi mkoani humo kujiunga kwenye ushirika kwani yapo mafaniko makubwa yanayopatikana kwa mtu kuwa kwenye ushirika wa kuweka na kukopa.
Boniface alisema ndani ya vyama vya ushirika yapo mafanikio mengi yanayopatikana hivyo aliomba watanzania kuhamasika kujiunga waweze kupata manufaa ya muda mfupi na mrefu.
Alisema vyama vya ushirika vipo vile vinavyojihusisha na kilimo, ufugaji, kuweka na kukopa vikiruhusu watanzania kujiunga navyo bila ya ubaguzi wowote ule.
Boniface alivitaja vyama vya ushirika ambavyo wameongozana navyo katika maonesho ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kuwa ni Chama Cha Ushirika Nyanza, FSA Mkolani Saccos na Rudea Saccos.
Ofisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Halmashauri ya jiji la Mwanza, Saguda Yohana alisema uwekaji wa akiba ndani ya vyama vya Ushirika humwezesha mtu kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo huwezesha biashara kukua haraka katika sekta za uzalishaji mali.
"Riba inayotozwa kwenye vyama vya ushrika ni kuanzia asilimia moja hadi 14" alisema Yohana.
Yohana alisema akiba hizo vilevile humpatia mwekezaji fursa ya kuwa mmiliiki wa hisa katika uwekezaji kwenye ushirika aliojiunga kuwa miongoni mwao na kulipwa faida inayopatikana kutokana na mtaji walio nao.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment