Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amewataka wananchi na wafanyabiashara kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na usafi wa mazingira wakati wote ili kulinda afya na kuboresha maeneo ya biashara badala ya kusubiri siku maalum.
Shekimweri aliyasema hayo juzi wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilipoadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya usafi katika Soko la Job Ndugai, akisisitiza kuwa mshikamano wa Watanzania ni msingi mkuu wa kulinda amani na maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi 971 kutoka JWTZ, Hamis Kinguye, alieleza kuwa walichagua soko hilo kutokana na kuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu unaohitaji usafi na usalama wa kiwango cha juu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano mwema kati ya jeshi na jamii kupitia shughuli za huduma kwa wananchi katika maadhimisho hayo ya miaka 62 tangu Septemba Mosi, 1964.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment