Idara ya Afya ya Jimbo la Pennsylvania nchini Marekani imetangaza vifo viwili vinavyohusiana na ugonjwa wa surua ambavyo vimetokea kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo kwa kipindi cha takriban miongo mitatu, huku vifo hivyo vikitajwa kuwahusu watu ambao hawakuwa wamepata chanjo.
Mlipuko huo mkubwa uliowakumba wagonjwa hao katika kaunti ya Lancaster umeambatana na kuwapo na watu karibu watu mia tano mwaka hu pekee ambaoi wana dalili zote za surua.
Kutokana na shida hiyo wataalamu wa agfya wanalazimika kutumia mbinu ngumu za nyumba kwa nyumba na ushawishi wa mdomo kwa mdomo kutoa elimu ya chanjo ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa maambukizi hayo yanayotajwa kuchochewa na wimbi la wananchi kusita kupokea chanjo.
Hata hivyo, kutangazwa kwa vifo hivi kumeibua mzozo mkubwa wa kiutendaji na kisiasa baada ya Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kusitisha kwa muda kuvijumuisha katika takwimu rasmi za kitaifa huku vikisubiri uchunguzi zaidi kubaini kama surua ndiyo iliyosababisha moja kwa moja vifo hivyo au wagonjwa walifariki kwa sababu nyingine za kiafya wakati wakiwa na maambukizi, hatua iliyozua malalamiko kutoka kwa maofisa wa afya wa jimbo hilo wanaosisitiza kuwa taratibu zote za kawaida za kitakwimu zilifuatwa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment