" VIONGOZI UWT WAHANI MSIBA WA MAREHEMU MAMA KARUME

VIONGOZI UWT WAHANI MSIBA WA MAREHEMU MAMA KARUME



NA: MWANDISHI WETU, Z'BAR

Viongozi wa kitaifa wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), wamefika kuhani msiba wa marehemu mama Fatma Karume. Viongozi hao wamefikisha salamu zao za pole, Mbweni, Zanzibar,  Septemba 30, 2026.

Akitoa salamu za pole, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, amesema marehemu mama Karume ni miongoni mwa waasisi wa UWT, ambaye mchango wake utakumbukwa na kuenziwa daima.

"Marehemu mama Karume alikuwa miongoni mwa waasisi walioweka msingi imara wa UWT ambapo leo wengine tunapita juu yake. Amechangia kubadili mtazamo wa wanawake kutoka kujiona viumbe duni hadi mashujaa na nguzo ya uhai wa Chama na maendeleo ya taifa kwa ujumla," amesema Chatanda.

Ameongeza kuwa, mama Karume enzi za uhai wake, amechangia ongezeko la idadi ya wanachama wanawake ambao awali walidhani wanawake si sehemu ya siasa na hivyo kuanza kushiriki shughuli za siasa.

"Zamani wanawake walikuwa na uoga na kukosa uthubutu wa kushiriki kikamilifu katika masuala ya siasa na uongozi, lakini kupitia mama Karume, wanawake wakapata ujasiri na leo tunao viongozi wengi wanawake ambao wanafanya vizuri katika uongozi kama alivyo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wengine wengi," amesema.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Zainabu Shomari, amesema UWT itaendeleza mema yote yaliyoasisiwa na mama Karume kwani ana mchango mkubwa katika maendeleo na Chama na taifa.


Naye, Katibu UWT Taifa, Suzan Kunambi, amesisitiza kuwa maendeleo yaliyopatikana Zanzibar, hayawezi kutenganishwa na mchango wake, ndiyo maana Jumuiya hiyo inasisitiza wanawake kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, ambaye ni miongoni mwa watoto wa marehemu, amewashukuru viongozi hao kwa kuja kuwapa pole na kutambua mchango wa mama Karume katika Jumuiya hiyo muhimu ya CCM.

Ikumbukwe kuwa, Mama Karume alifariki Septemba 21, 2026, akiwa nyumbani kwake Mbweni, visiwani humo, ambapo amefariki akiwa na umri wa miaka 97.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652




Post a Comment

Previous Post Next Post