Diwani wa kata ya Mwagi Wilaya ya kwimba Mkoani Mwanza Masumbuko Shigita amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama kutokana na tishio la kutokea kwa mvua za Elmino.
Ziara hiyo ya kutembelea kata hiyo ilienda sambamba na kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo na kusisitiza juu ya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama rasmi .
Akizungumza leo na wananchi wa kata ya Mwagi alieleza namna ambavyo serikali inaendelea kutekeleza miradi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kisima cha maji na nguzo za umeme.
Martini Erasto ametoa pongezi kwa diwani pamoja na mbunge wa Jimbo la Sumve kwa namna ambavyo wamekuwa wakijitoa kwa ajili ya kutatua kero za wananchi na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Wananchi wa kata ya Mwagi walipata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo.
Walisema utashi huo ni ishara ya kwamba viongozi wanatambua nafasi zao.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment