" ENG.CHILOMBE NA AHADI YA MADARASA 60 MAPYA KUPITIA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

ENG.CHILOMBE NA AHADI YA MADARASA 60 MAPYA KUPITIA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

 


MBUNGE wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe, amewataka wananchi wa Kijiji cha Lukumbo, Kata ya Nalasi Mashariki, kuwa na imani naye katika utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni, akisisitiza kuwa ataendelea kuzitekeleza kwa hatua mbalimbali.

Chilombe ametoa kauli hiyo baada ya kusimamishwa na wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara katika Kijiji cha Lukumbo, ambapo amewaeleza kuwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, anakusudia kutumia rasilimali hizo kimkakati katika kuboresha huduma za elimu katika maeneo mbalimbali ya jimbo.

Amesema moja ya vipaumbele vyake ni ujenzi wa madarasa mapya 60, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani, sambamba na ukarabati wa miundombinu ya madarasa ambayo imechakaa.

Aidha, Mbunge huyo amewaahidi wananchi wa Lukumbo kuwa katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha kijiji hicho kinapata zahanati mpya yenye hadhi, ili wananchi waweze kupata huduma za afya karibu na maeneo yao bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.

Chilombe amesisitiza kuwa utekelezaji wa ahadi hizo utafanyika kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi na mahitaji halisi ya maeneo mbalimbali ya Jimbo la Tunduru Kusini.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652


Post a Comment

Previous Post Next Post