" WEKENI VIAKISI MWANGA KWENYE BAJAJI ZA MIZIGO

WEKENI VIAKISI MWANGA KWENYE BAJAJI ZA MIZIGO


Madereva wa bajaji za mizigo katika eneo la Phantom Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu umuhimu wa kubandika utepe ang'avu kwenye bajaji hizo.

Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Sajenti Ibrahimu Lukumbo amewaeleza madereva hao kuwa utepe ang'avu unasaidia chombo hicho Cha moto kuonekana Kwa urahisi nyakati za usiku na kuepuka na ajali za barabarani.

Sajenti Lukumbo amewafafanulia kuwa matumizi ya bajaji za mizigo zisizokuwa na utepe ang'avu hushindwa kuonekana Kwa urahisi na kuwa Moja ya visababishi vya ajali za barabarani.

Madereva hao walionufaika na elimu hiyo wamelishukuru Jeshi la Polisi Kwa kuwafikiahia elimu hiyo na kuahidi kushirikiana vema na Jeshi la Polisi ili kutokomeza ajali zinazoweza kuepukika.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 03

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post