Amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa ni tunu muhimu zinazopaswa kulindwa na kila Mtanzania, huku viongozi wa vyama vya siasa wakitakiwa kuwa mstari wa mbele kuzilinda kutokana na ushawishi mkubwa walionao katika jamii.
Viongozi hao, wawe wa chama tawala au vyama vya upinzani, wana wajibu wa kuhakikisha kauli wanazozitoa zinakuwa sehemu ya kujenga taifa badala ya kuligawa, kwani kila neno wanalozungumza mbele za wananchi husikilizwa na watu wengi na linapaswa kupimwa kwa kuzingatia athari zake kwa jamii.
Ingawa ni jambo la kawaida katika demokrasia kuwa na mitazamo na misimamo tofauti inayochochea ushindani wa kisiasa, tofauti hizo hazipaswi kamwe kugeuka kuwa chuki, uhasama, matusi, vitisho au uchochezi unaoweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Hivi karibuni, Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania lilitoa angalizo hilo kwa kuwataka viongozi wa siasa kuwa makini na kuchunga kauli wanazozitoa, huku Mwenyekiti wa baraza hilo, Juma Ali Khatib, akisisitiza kuwa chanzo cha machafuko yoyote mara nyingi huanzia kwenye kauli na kuahidi kukutana na viongozi wa vyama vyote ili kuendelea kukemea lugha za uchochezi.
Jitihada hizi za kuwakutanisha viongozi katika majadiliano zinapaswa kupewa kipaumbele na kuendelezwa ili kupunguza tofauti, kujenga uaminifu miongoni mwa wadau, na kulinda sifa ya Tanzania kama nchi ya amani inayowaruhusu wananchi wake kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii bila hofu.
Aidha, viongozi wa kisiasa wametakiwa kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwani kauli zinazotolewa kwa hasira au kwa lengo la kutafuta umaarufu zinaweza kusambaa kwa kasi na kuchochea hisia mbaya miongoni mwa wananchi, jambo linaloashiria kuwa uhuru wa kutoa maoni unapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji mkubwa.
Sambamba na hilo, vijana hawapaswi kutumiwa kama nyenzo ya migogoro ya kisiasa, bali viongozi wanapaswa kuwahamasisha kushiriki katika siasa za hoja, kujenga uchumi na kutafuta fursa za maisha, huku wakitanguliza maslahi ya Taifa mbele ya maslahi binafsi au ya vyama vyao kwa kuwa ushindi wa kisiasa unapita lakini Tanzania na watu wake wataendelea kuwepo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment