" ARUSHA ARTSAN FESTIVAL YAIBUA FURSA MPYA KWA WASANII.

ARUSHA ARTSAN FESTIVAL YAIBUA FURSA MPYA KWA WASANII.

 


Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.

BASATA Yawataka Wasanii Kujisajili, Kuchangamkia Fursa za Masoko

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za ufundi na masoko Bona Masenge akimuwakilisha Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Tourism Festival (TITF), Ibrahim Jama kwa kuandaa tamasha la wabunifu na wasanii Arusha (AAF) akisema tamasha hilo limeunganisha kwa pamoja sanaa, utamaduni, utalii, biashara na uchumi wa ubunifu.

Akifungua tamasha hilo  amesema Arusha ni miongoni mwa maeneo yenye nafasi muhimu katika utalii, mikutano, biashara, utamaduni na mahusiano ya kimataifa, hivyo tukio hilo ni jukwaa muhimu la kuonyesha uwezo wa Tanzania na thamani ya bidhaa zinazotengenezwa na Watanzania.


Aidha amesema mafundi sanaa na wasanii hawapaswi kuonekana kama watu wanaotengeneza bidhaa za mapambo pekee, bali ni wajasiriamali, wabunifu na watunzaji wa utamaduni wa Tanzania wanaochangia ajira na kipato kwa familia na jamii.

Amesema "Serikali na wadau wanapaswa kuhakikisha wasanii wanapata masoko, ujuzi, teknolojia, mitaji na haki miliki. Mfuko wa Utamaduni na Sanaa umeanzishwa kuwawezesha wajasiriamali na wabunifu kuongeza mitaji na kukuza shughuli zao".

Amewataka wasanii kutumia fursa hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kujisajili BASATA na kutambulika na taasisi nyingine muhimu kama COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa 


Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Tourism Festival (TITF), Ibrahim Jama ameiomba serikali kulinda haki za wasanii, kuwawezesha kushiriki maonyesho nje ya nchi Kwa lengo la kukuza mtandao wa biashara zao, kupata ujuzi na masoko ya uhakika.

Amesema kuwa washiriki 100 wakiwawakilisha maelfu ya wanasanaa nchini wameshiriki wameshiriki maonyesho hayo, yanayolenga kuibua fursa za kiuchumi katika sekta ya utalii wa Sanaa. Amesema utalii wa Sanaa umekuwa nguzo mhimu ya ukuaji wa uchumi na kuingiza Dola za kimarekani milioni 500 kila mwaka 

Amesema "Tunaamini kwamba tuna mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania, ni wakati muafaka sasa kupata mialiko kupitia vyama shirikishi ambavyo viko nchini lakini pia na Baraza la Sanaa Wahakikishe wasanii hawa wanaeshimika na  kuaminiwa".

"Ni wakati wao wa kutambulika kuwa  kazi zao zimechorwa na nani, zimechorwa muda gani, nani aliweza kuchora sanaa hizi, nani aliweza kuwa fundi wa sanaa hizi" amesema Ibrahim".

Vilevile amesema kazi za wasanii  zimekuwa zikinunuliwa Kwa bei ndogo na kwenda kuuzwa nje ikiwemo Marekani na Uingereza. Hatua hiyo imekuwa ikiwarudisha nyuma wasanii Kwa sababu ya kukosa fursa ya kuuza bidhaa zao wenyewe nje ya nchi.

Katika namna hiyo hiyo Katibu wa wanasanaa wa Masai market Zainab Kahimba amepongeza hatua ya kufanyika kwa tamasha hilo Jijini Arusha ambalo amelitazamia kama mlango wa fursa za kiuchumi na kutangaza bidhaa zao.


Zainabu ameiomba serikali kuwatangazia Bunge la Mabunge Duniani (IPU) linaloendelea Arusha kufika katika viwanja vya General tyre Njiro-Arusha kununua bidhaa za Sanaa na kufurahia utalii wa uchongaji.

Mwenyekiti wa chama cha wachongaji Sanaa nchini CHAWASAWATA Sebastian Daniel amesema wanasanaa wamekuwa ni watu wa kubaki nyuma muda wote hali inayopelekea kudharaulika Kwa tasnia hiyo.

"Umefika wakati wetu kuamka na kuchangamkia fursa zilizopo mbele yetu, tujisajili katika chama Ili tuweze kushirikiana kudai haki zetu" amesema.

PROFESSOR MGOKO EP 04

Post a Comment

Previous Post Next Post