Mbunge wa Jimbo la Uyole ambae ni Rais wa Heshima wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe Dkt. Tulia Ackson ametimiza ahadi yake kwa kijana anayesumbuliwa na changamoto ya ulemavu wa miguu kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la James Nelson Kilasi kwa kumsaidia kiti mwendo cha umeme.
James ni kijana anayeishi kata ya Igawilo mtaa wa Chemchem ambaye changamoto hii imemsumbua kwa muda mrefu na hapo awali alikosa msaada wa kutatua changamoto hiyo hadi pale taarifa ilipo mfikia Dkt. Tulia.
Kupitia tamasha la Ngoma za Asili linalojulikana Kama Tulia Traditional Dancer Festival 2026 lililofanyika hivi karibu uwanja wa shule ya msingi Gombe Mh. Dkt. Tulia alipata taarifa ya kijana James kuhusu changamoto zake na kupitia mama mzazi wa kijana huyo na kuhaidi kuitatua.
Bi. Hellberitha Ephraim ambaye ni mama mzazi wa James amemshukuru Mh. Dkt. Tulia kwa kumsaidia mtoto wake kupata kiti mwendo kitakacho msaidia wakati wa kwenda na anapokuwa chuoni kuendelea na masomo yake.
PROFESSOR MGOKO EP 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment