" ENABEL YAONGEZA MAKALI, KALAMU ZAGEUKA KUWA SILAHA DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

ENABEL YAONGEZA MAKALI, KALAMU ZAGEUKA KUWA SILAHA DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Katika jitihada za kupambana na kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia nchini, Shirika la Enabel kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Kasulu limehamasisha ushiriki wa wanafunzi kupitia shindano la ubunifu lililolenga kuwapa vijana nafasi ya kuibua ujumbe na mawazo ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.Katika shindano hilo, Erick Cornely kutoka Shule ya Sekondari Kinkati ameibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika Halmashauri ya Mji Kasulu na mshindi wa kwanza shuleni hapo  baada ya kuwasilisha mchoro unaoonesha chanzo cha ukatili na namna ya kuutokomeza  huku nafasi ya pili kwa upande wa shule hiyo ikichukuliwa na Gaspar Alex.Kwa upande wa Shule ya Sekondari Kigodya, Josin Yotham Bukuru ameibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Ngoga Haja aliyeshika nafasi ya pili kwa  ngazi ya shule hiyo.Aidha, Shule ya Sekondari Nyasha, Twaha Abdallah ameshika nafasi ya kwanza  huku Beatrice Japhary akishika nafasi ya pili baada ya kuchira  mchoro unaoonesha namna ya kutambua vitendo vya ukatili na kuviepuka.Wanafunzi walioshiriki wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo madaftari (counter books), kalamu, compass na begi kwa mshindi wa kwanza wa jumla huku wakihimizwa kutumia vipaji na ubunifu wao kuelimisha jamii kuhusu madhara ya unyanyasaji wa kijinsia na umuhimu wa kuzuia vitendo hivyo.Shindano hilo limewapa wanafunzi nafasi ya kushiriki na kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii za kupinga unyanyasaji wa kijinsia likisisitiza matumizi ya elimu, vipaji na ubunifu kama nyenzo za kuleta mabadiliko chanya katika jamii


 

Post a Comment

Previous Post Next Post