Madereva wa Magari ya abiria wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu uendeshaji wa tahadhali ili kujiepusha na ajali hasa tunapoelekea kipindi Cha El nino.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika Stendi kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga ambapo amewaeleza madereva hao kuwa wanapaswa kujipanga vema kipindi Cha mvua nyingi wanapokuwa barabarani kuepukana na ajali za mara Kwa mara.Sajenti Ndimila amewasisitiza madereva hao kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kusababisha ajali kipindi Cha mvua nyingi kama kupitisha gari kwenye maji mengi pasipo kujua kina Cha maji hayo, kuepuka kufunga breki za ghafla, kuwasha taa wakati wa mvua ili kuweza kuona mbele na kuonekana na watumiaji wengine wa barabara, kuepuka mwendo Kasi pamoja na kuacha nafasi ya kutosha katika ya gari Moja na jingine wawapo barabarani.Aidha amewaeleza kuwa endapo watatimiza wajibu wao pasipo shuruti watafanikiwa kusafirisha abiria katika mazingira salama pamoja na kupunguza matukio ya ajali za barabarani yanayoweza kuepukika.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment