" KAMPENI YA ONGEA NA KAMANDA YAWAFIKIA KAGONGWA WAPEWA ELIMU YA AMANI, UKATILI NA USALIMISHAJI WA SILAHA HARAMU

KAMPENI YA ONGEA NA KAMANDA YAWAFIKIA KAGONGWA WAPEWA ELIMU YA AMANI, UKATILI NA USALIMISHAJI WA SILAHA HARAMU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, ametoa elimu kwa wananchi wa Kata za Wendele na Kagongwa, Wilaya ya Kahama, kuhusu umuhimu wa kulinda amani, kuripoti matukio ya ukatili na kusalimisha silaha haramu kabla ya muda uliowekwa kumalizika.

Katika kampeni ya Ongea na Kamanda, SACP Magomi amewakumbusha wananchi kuwa dhamana haitolewi kwa kulipia fedha, huku wanaume akiwahimiza kutokuwa na hofu ya kuripoti matukio ya ukatili wanayofanyiwa au kuyashuhudia ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Aidha, amewataka wananchi wanaomiliki silaha haramu kuzisalimisha katika ofisi za Serikali za vijiji na mitaa, ofisi za watendaji wa kata au vituo vya polisi kabla ya Oktoba 31, 2026, ambayo ndiyo tarehe ya mwisho ya kampeni hiyo, akionya kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuendelea kumiliki silaha hizo baada ya muda huo kumalizika.

Katika mikutano hiyo, wananchi waliwasilisha changamoto mbalimbali, zikiwemo ugumu wa madereva wa bajaji kupata leseni kutokana na gharama za mafunzo katika vyuo vya udereva, pamoja na uhitaji wa makoti ya mvua kwa askari wa ulinzi shirikishi wa Sungusungu katika Kata ya Wendele kuelekea msimu wa masika.

Akijibu changamoto hizo, OCD wa Kahama alieleza kuwa atatoa makoti 10 ya mvua kwa Sungusungu wa Kata ya Wendele siku hiyo, ili kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama wakati wa mvua.

Kuhusu changamoto ya leseni za madereva wa bajaji, OCD wa Kahama kwa kushirikiana na Afisa wa Polisi anayeshughulikia masuala ya usalama barabarani (DTO), watawasiliana na vyuo vya udereva ili kutafuta utaratibu wa kuwasajili madereva hao kwa gharama nafuu, waweze kupata mafunzo na vyeti vinavyohitajika ili kukidhi masharti ya kupata leseni.

Kupitia kampeni hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea kuhimiza ushirikiano na wananchi katika kulinda amani, kuzuia uhalifu na kuhakikisha matukio ya ukatili yanaripotiwa kwa wakati ili hatua stahiki zichukuliwe.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 06

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post