Wazee wa Halmashauri ya Mji Kasulu wameshiriki warsha kuhusu haki za wazee na sheria zinazowalinda nchini Tanzania, iliyolenga kutoa elimu ya sheria, kuainisha mfumo wa rufaa na kuimarisha ulinzi wa wazee katika Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.Warsha hiyo imeandaliwa na shirika la HelpAge Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI), imefanyika katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kasulu.Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Mgeni Rasmi Ibrahim Mwangalumu amewataka wazee kutekeleza maazimio ya warsha hiyo, ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa mara, kutangaza huduma za kliniki za wazee na kuhuisha mabaraza yote.Wakiwasilisha mada katika warsha hiyo, Meneja Miradi wa HelpAge Tanzania, Bw. George Ouma na Naibu Mkurugenzi wa EWAKI Bw. Frank Baseka, wameihimiza jamii kutambua na kuheshimu haki za wazee hususan haki ya kulindwa dhidi ya ukatili na haki ya kumiliki mali.Aidha, wameiomba Serikali kuweka mifumo madhubuti ya kuwahudumia wazee, kuanzisha madawati maalumu na kuwajumuisha wazee katika fursa mbalimbali ikiwemo mikopo inayotolewa na Halmashauri.Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Yohane Mgaya amesema mfumo wa rufaa unasaidia kutambua wadau muhimu, kuelewa hatua za ufuatiliaji wa rufaa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa na kuimarisha ushirikiano. Halmashauri ya Mji Kasulu imeahidi kuendeleza mikakati yake ya kutoa elimu kuhusu haki na ustawi wa wazee kupitia mikutano ya Kata na vyombo vya habari.Kauli mbiu ya Warsha hiyo inasema “Uzee na Kuzeeka, Haukwepeki.”
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment