" MWENYEKITI WA MISA TAN AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI

MWENYEKITI WA MISA TAN AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika - Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), Edwin Soko, amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kuzingatia maadili ya taaluma na kutumia nafasi zao kuibua fursa mbalimbali za maendeleo kwa jamii.

Soko ametoa rai hiyo leo Oktoba 12, 2026 jijini Mwanza wakati akifungua kongamano la MISA Tanzania lililowakutanisha wahariri, waandishi wa habari na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na sekta binafsi, kwa lengo la kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya tasnia ya habari na wadau hao.

Akizungumza katika kongamano hilo, Soko amesema MISA Tanzania inatambua umuhimu wa wadau kutoka sekta mbalimbali kutokana na mchango wao katika kuendeleza tasnia ya habari, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga mazingira ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Kongamano hilo limewakutanisha zaidi ya wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kati, pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Idara ya Uhamiaji, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Daniel Machunda, aliyewasilisha salamu kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza MISA Tanzania kwa kuwakutanisha wadau hao na kusisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuendelea kubaini na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo.

Machunda amesema ushirikiano kati ya waandishi wa habari na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuifikishia jamii taarifa zenye manufaa, kuongeza uelewa wa wananchi na kuibua fursa zinazoweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kongamano hilo limekuwa jukwaa la kukutanisha wanachama wa MISA Tanzania na wadau kutoka sekta mbalimbali, kwa lengo la kubadilishana mawazo, kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 05

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post