Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Azizi Kirondomara, akizungumza wakati wa kongamano la MISA Tanzania lililowakutanisha wanachama wa taasisi hiyo na wadau mbalimbali jijini Mwanza.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Azizi Kirondomara, amewataka Watanzania kuwa na utaratibu
wa kuomba pasipoti za kusafiria mapema badala ya kusubiri hadi wanapopata
safari za kwenda nje ya nchi, ili kujiandaa kwa wakati na kuepuka usumbufu
unaoweza kujitokeza wakati wa maandalizi ya safari.
Kirondomara
ametoa wito huo wakati wa kongamano la MISA Tanzania lililowakutanisha
wanachama wa taasisi hiyo pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Serikali
na sekta binafsi jijini Mwanza, akisisitiza umuhimu wa Watanzania kuzingatia
maandalizi ya mapema kwa safari za kimataifa.
Aidha,
amewashauri Watanzania ambao tayari wana pasipoti kuhakikisha wanazitunza kwa
usalama na kuepuka kutembea nazo bila sababu za msingi, akieleza kuwa baadhi ya
watu wamekuwa wakipoteza nyaraka hizo wanapokuwa wanazibeba bila kuwa na safari
inayohitaji matumizi yake.
Amesisitiza
kuwa pasipoti ni nyaraka muhimu kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya
nchi, hivyo ni muhimu kuzihifadhi vizuri na kufuata taratibu za Idara ya
Uhamiaji ili kuhakikisha zinakuwa salama na zinapatikana pale zinapohitajika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, ameeleza umuhimu wa kuwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali katika shughuli za wanahabari, akibainisha kuwa ushirikiano huo unasaidia kuongeza uelewa wa masuala yanayohusu huduma na majukumu ya taasisi hizo nchini.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Azizi Kirondomara, akiwasilisha taarifa kuhusu huduma na majukumu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa kongamano la MISA Tanzania jijini Mwanza.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















































































































Post a Comment