Wananchi wa Kata ya Ruhita,Halmashauri ya Mji Kasulu, Mkoni Kigoma wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara kupokea taarifa ya Serikali kutoa zaidi ya shilingi milioni 838.612 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo jirani.Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Ayubu Ngalaba Kilugu, amewataka wananchi kuthamini juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo na kushirikiana na viongozi kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kwa mafanikio. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nurfus Azizi Ndee, amewahimiza wananchi kushiriki katika maandalizi ya ujenzi ikiwemo usafishaji wa eneo la mradi.Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Nangi W. Nangi, amewahimiza wananchi kutumia fursa ya Bima ya Afya kwa Wote ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu huku akisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko yakiwemo kipindupindu pamoja na ugonjwa wa Ini.Kwa upande wao, wananchi wameishukuru Serikali kwa kutenga fedha hizo, wakieleza kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutapunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za afya na kuahidi kushirikiana na viongozi katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment