Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo, amesema baraza la
madiwani limeweka vipaumbele vya kuboresha huduma za afya, miundombinu ya
barabara pamoja na miundombinu ya elimu ili kuhakikisha wananchi wanapata
huduma bora na wanafunzi wanasoma katika mazingira salama na rafiki.
Kitumbo
ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga uliojadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kutoka
katika kata za manispaa hiyo.
Amesema
katika kutekeleza vipaumbele hivyo, ni muhimu madiwani kuhakikisha wanasimamia
ipasavyo fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kata zao
ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa
wananchi.
Aidha,
amezihimiza taasisi za huduma za kijamii ikiwemo Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) pamoja
na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuweka utaratibu wa
kushiriki katika vikao vya vya madiwani.
Amesema
ushiriki wa taasisi hizo utasaidia kujadili changamoto zinazowakabili wananchi
katika maeneo mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja kabla hazijawa
kubwa zaidi.
Katika
mkutano huo, baadhi ya madiwani wamewasilisha changamoto zinazowakabili
wananchi katika kata zao, zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya barabara ikiwemo
Kata ya Ngokolo, Ndembezi na Kolandoto.
Pia, wameeleza
kutoridhishwa na hali ya miundombinu ya umeme katika baadhi ya maeneo ya
manispaa hiyo, wakitaja Kata za Mwamalili, Old Shinyanga, Chibe, Kizumbi na
Kitangili kuwa miongoni mwa maeneo ambayo bado yanahitaji kuongezewa huduma
hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Salum Kitumbo, akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo uliojikita katika kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za kijamii na miundombinu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Salum Kitumbo, akiwa pamoja na viongozi wengine katika meza kuu wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ndembezi, Mhe. Pendo Sawa, akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani uliojadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika kata za manispaa hiyo.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea na mkutano wake wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika kata, kubainisha mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Salum Kitumbo, akiwa pamoja na viongozi wengine katika meza kuu wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Mwamalili Mhe. James Matinde Mdimi , akielezea mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata yake wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa viti maalum tarafa ya Mjini Mhe. Veronica Masawe akielezea mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata yake wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa Kata ya Kizumbi Mhe. Reuben Kitinya, akielezea mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata yake wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hoja na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea na mkutano wake wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika kata, kubainisha mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hoja na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hoja na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hoja na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kwa makini hoja na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Kolandoto Mhe. Moses Mshagatila, akielezea mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata yake wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli Mhe. Zuhura Waziri, akielezea mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata yake wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
























Post a Comment