" ACT WAZALENDO SHINYANGA YAFUNGUA DIRISHA LA KUWANIA NAFASI YA MWENYEKITI WA MKOA

ACT WAZALENDO SHINYANGA YAFUNGUA DIRISHA LA KUWANIA NAFASI YA MWENYEKITI WA MKOA

 Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga kimetangaza kuanza kwa zoezi la uchukuaji fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya mkoa, ambayo imekuwa wazi kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga, Hassan Ibrahim, ambaye amesema hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa kumpata mwenyekiti mpya atakayekiongoza chama hicho mkoani humo.

Amesema zoezi la uchukuaji fomu litaanza Novemba 30, 2026, hadi Desemba 8, 2026, kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sifa za mwombaji ni kuwa Mtanzania, mwanachama hai wa ACT Wazalendo, awe anajua kusoma na kuandika, pamoja na kuwa na akili timamu.

Fomu za kuwania nafasi hiyo zinapatikana katika Ofisi ya Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga.

Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga kina majimbo manne ya uchaguzi ambayo ni Kishapu, Shinyanga Mjini, Itwangi na Solwa.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 08

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post