Na Mapuli Kitina Misalaba
Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) kuharakisha usanifu wa kina wa barabara
inayounganisha Halmashauri ya Ushetu na Kahama ili iweze kuingizwa katika
mipango ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Maelekezo
hayo yametolewa Novemba 11, 2026, wakati Waziri Mkuu akizungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi ya Nyamilangano,
Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga, baada ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe.
Emmanuel Peter Cherehani, kuwasilisha changamoto ya barabara hiyo na kuomba
ijengwe kwa kiwango cha lami.
Akitoa
ufafanuzi, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Ntuli Mwaikokesye, amesema
usanifu wa kina wa barabara hiyo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi minne.
Hata hivyo,
Dkt. Mwigulu amemtaka meneja huyo kuongeza kasi ya kazi kwa kufanya kazi usiku
na mchana ili kupunguza muda wa kukamilisha usanifu huo na kuiwezesha Serikali
kuzingatia mradi huo katika maandalizi ya bajeti ijayo.
Katika hoja
nyingine, Mbunge Cherehani amewasilisha changamoto ya gharama za tozo na riba
zinazohusiana na upatikanaji wa pembejeo za kilimo, hususan kwa wakulima wa
tumbaku, akieleza namna gharama hizo zinavyoongeza mzigo kwa wakulima.
Akijibu hoja
hiyo, Waziri Mkuu amewaelekeza Mawaziri wenye dhamana ya TAMISEMI, Fedha na
Kilimo kukaa pamoja na kupitia upya muundo wa tozo hizo ili kubaini namna ya
kupunguza gharama zinazowakabili wakulima. Amesema atashirikiana na mawaziri
hao pamoja na wabunge wa maeneo yanayokabiliwa na changamoto hiyo kutafuta
ufumbuzi.
Kuhusu
changamoto ya kukatika kwa umeme, Dkt. Mwigulu amesema hali hiyo inahusishwa na
ongezeko la matumizi ya umeme kufuatia upanuzi wa huduma katika maeneo mengi,
ambao umeongeza mahitaji kwenye miundombinu ya gridi ya taifa.
Ametoa mfano
wa huduma ya umeme iliyokuwa imepangwa kufika Kahama lakini sasa imeendelea
kusambazwa hadi maeneo ya vijijini, hali inayoongeza mahitaji ya umeme katika
mfumo wa usambazaji.
Waziri Mkuu
amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mradi wa Gridi Imara wenye thamani ya
zaidi ya Shilingi trilioni 1.1, ambao unalenga kuimarisha uwezo wa kusafirisha
na kusambaza umeme ili kukidhi ongezeko la mahitaji nchini.
Aidha,
ameelekeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kuwaunganishia umeme
wananchi wanaostahili gharama ya Shilingi 27,000, akisisitiza kuwa hadhi ya
kiutawala ya eneo isiwe sababu ya kuwatoza wananchi gharama kubwa wakati
mazingira yao bado yanafanana na vijijini.
Katika ziara
hiyo, Dkt. Mwigulu amesisitiza pia umuhimu wa kusimamia thamani ya fedha
zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,
akieleza kuwa fedha hizo zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na
miradi ikamilishwe kwa ubora unaotakiwa.
Mkutano huo
umetoa nafasi kwa wananchi wa Ushetu kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja
kwa Waziri Mkuu, huku viongozi na watendaji wa Serikali wakipata maelekezo ya
kushughulikia hoja zilizowasilishwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Ushetu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Novemba 11, 2026, ambapo alisikiliza kero mbalimbali na kutoa maelekezo ya kuzitatua.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba na wananchi wa Halmashauri ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Peter Cherehani, akiwasilisha changamoto za wananchi wa jimbo hilo mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, ikiwemo ujenzi wa barabara ya Ushetu–Kahama kwa kiwango cha lami.
Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Ushetu wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, uliotoa fursa ya kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Ushetu wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, uliotoa fursa ya kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Ushetu wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, uliotoa fursa ya kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



































Post a Comment