Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kigoma imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Kasulu, kwa lengo la kutathmini maendeleo ya utekelezaji wake na kujiridhisha na ubora wa kazi zilizofanyika.Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kigodya, vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Ruhita, ujenzi wa shule mpya za msingi Kabanga Mazoezi na Mwibuye, ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Heru Juu pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Kimobwa.Akiongoza ziara hiyo, SACP Filimon K. Makungu, amewataka wasimamizi na watekelezaji wa miradi kuwajibika ipasavyo kwa kuzingatia weledi, ubunifu na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi na kwa viwango vinavyotakiwa.Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa miradi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za manunuzi ya umma ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyowekwa.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia J. Simbeye, ameishukuru Kamati hiyo kwa ushauri na maelekezo iliyoyatoa huku akiahidi kuyafanyia kazi ili kuimarisha usimamizi na kuhakikisha miradi inakamilika kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa.Ziara hiyo imefanyika tarehe 05 Novemba 2026 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha miundombinu ya elimu kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment