" MWANAUME AKUTWA AMEFARIKI NDANI MOROGORO

MWANAUME AKUTWA AMEFARIKI NDANI MOROGORO

 


Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Halidi, mkazi wa Mtaa wa Kambi Tano, Kata ya Lukobe katika Manispaa ya Morogoro, amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba ya mjomba wake aliyokuwa akiishi, huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Eliamini Kimaro, ameeleza kuwa waligundua tukio hilo kufuatia taarifa za majirani waliopata mashaka baada ya kusikia harufu kali ikitoka ndani ya chumba chake, ambapo walikuta mwili wake ukiwa tayari umeanza kuharibika.
Kwa mujibu wa majirani, marehemu alikuwa hajaonekana mtaani hapo kwa takribani siku tatu kabla ya kukutwa kwa mwili wake akiwa amefariki.
Majirani hao wamebainisha kuwa Halidi alikuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali za mjini, huku wakieleza kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia vileo vikali licha ya kukabiliwa na changamoto ya maradhi ya figo.

 PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post