MAISHA YAKO NA YA WENGINE NI MUHIMU. Askari Polisi kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ametoa elimu kwa maafisa usafirishaji wa Kituo cha Ally’s Star kilichopo Manispaa ya Shinyanga, kuhusu umuhimu wa kuzingatia taratibu sahihi za kupita magari (Overtaking), kwa kutumia upande wa kulia badala ya kushoto, ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na makosa hayo.Katika elimu hiyo, madereva wamekumbushwa umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuchukua tahadhari na kuhakikisha njia iko salama kabla ya kufanya kitendo cha kupita gari jingine.Kwa upande wao, baadhi ya madereva waliopokea elimu hiyo wameahidi kuzingatia maelekezo hayo na kuyafanyia kazi kwa vitendo, kwa lengo la kupunguza ajali na kulinda maisha ya abiria pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment