" TAKUKURU MBEYA YAREJESHA MILIONI 82.9 ZA FEDHA ZA UMMA, YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI UBADHIRIFU

TAKUKURU MBEYA YAREJESHA MILIONI 82.9 ZA FEDHA ZA UMMA, YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI UBADHIRIFU

 

Naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Jasper Luoga akitoa taarifa kwa vyombo vya habari

Na Lydia Lugakila- Misalaba Media,MBEYA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya imefanikiwa kurejesha jumla ya shilingi milioni 82.9 zilizohusishwa na ubadhirifu pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma katika maeneo mbalimbali mkoani humo, huku ikiweka mikakati mipya ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 5, 2026, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga, amesema fedha hizo zimepatikana kufuatia hatua za uchunguzi na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma kwa lengo la kuhakikisha zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Alitaja baadhi ya matukio yaliyobainika kuwa ni pamoja na shilingi milioni 3,549,000 zilizohusishwa na ubadhirifu wa mifuko 42 ya mbolea katika Chama cha Ushirika cha Wakulima (AMCOS) cha Buseka, Runge.

Pia alitaja shilingi milioni 1,128,950 zilizohusishwa na mapato ya mashine za POS pamoja na makusanyo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela.


Katika tukio jingine, Luoga alisema Daniel Thomas Mwanakatwe alitumia kwa manufaa yake binafsi shilingi milioni 15,205,000 zilizochangwa na wanachama wa kikundi cha Asante Mbeya kwa ajili ya kununua gari aina ya Coaster.

Alieleza kuwa fedha hizo zilikuwa zimekusanywa kwa lengo maalumu la kununua gari kwa ajili ya kikundi hicho, lakini zilitumika kinyume na madhumuni yaliyokusudiwa.

Katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, TAKUKURU Mkoa wa Mbeya imeweka mikakati ya utekelezaji kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya rushwa na kuwafikia wadau kutoka makundi mbalimbali katika jamii.

Mikakati mingine ni kuendelea kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali ili kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, pamoja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kujihusisha na ubadhirifu au matumizi mabaya ya mali za umma.

Aidha, TAKUKURU imetoa wito kwa viongozi na watendaji wa umma kusimamia fedha za Serikali kwa kuzingatia misingi ya uwazi na uadilifu.

Hata hivyo Luoga amewahimiza Wananchi kufuatilia matumizi ya fedha za umma na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapobaini viashiria vya ubadhirifu au matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali za Serikali.

 PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment

Previous Post Next Post