" TANESCO RUVUMA YANG'ARA TUZO ZA UCHUMI GALA AWARDS

TANESCO RUVUMA YANG'ARA TUZO ZA UCHUMI GALA AWARDS


 
Afisa Msaidizi wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma, Emma Ulendo, amekabidhiwa tuzo maalum ya heshima na ubora katika utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Ulendo amesema tuzo hiyo ni ishara ya kutambua juhudi na kazi kubwa zinazofanywa na kitengo kizima cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja cha TANESCO katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora pamoja na elimu kuhusu matumizi ya nishati safi.


Aidha, amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akisisitiza kuwa kujituma, kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwajibika ni misingi muhimu ya kufikia mafanikio katika utendaji kazi.


Uchumi Gala Awards ni jukwaa linalolenga kutambua, kuthamini na kuenzi mchango wa wajasiriamali, wawekezaji, watu binafsi, taasisi na makampuni mbalimbali katika kukuza maendeleo ya jamii na uchumi wa Taifa kupitia uwekezaji, uundaji wa ajira na upatikanaji wa fursa endelevu za kipato.

 PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post