KARISMATIKI KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA WATAKIWA KUWA KIELELEZO CHA IMANI NA MAFUNDISHO YA KANISA
Misalaba0
Kikundi cha sala cha Karismatiki Katoliki jimbo la Shinyanga, kimetakiwa kuendelea kuilinda na kuitetea imani Katoliki, kupitia karama mbalimbali ambazo Mungu amewajalia wanachama wa kikundi hicho.
Wito huo umetolewa leo na Katibu wa Askofu wa jimbo katoliki Shinyanga Padre Deudedith Kisumo, wakati akiongoza adhimisho la Misa takatifu ya kilele cha Jubilei ya Miaka 25, tangu kuanzishwa utume wa kikundi hicho katika Jimbo la Shinyanga , iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Padre Kisumo ambaye alikuwa amemwakilisha Askofu wa jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewataka Wakarismatiki wote bila kujali karama zao kuwa wakomavu katika imani na mafundisho ya Kanisa, pamoja na kuwa kielelezo cha imani ya kweli kwa watu wengine hasa waliopotea.
Naye Padre Peter Bahati wa Shirika la Rosmini kutoka Jimbo Katoliki Tanga, ambaye alikuwa ni mmoja wa wawezeshaji katika kongamano la jubilei, ametumia mahubiri yake kutahadharisha juu ya matumizi mabaya ya maandiko matakatifu, hasa katika kile kinachoolezwa kunena kwa Lugha na kwamba, nguvu na kazi za roho mtakatifu zinapaswa kuheshimiwa bila kutiliwa chumvi kama baadhi wanavyofanya kwa lengo la kujipatia utukufu.
Misa ya kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya utume wa Karismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga, imehudhuriwa na Mapadre, Watawa, Viongozi wa Karismatatiki Katoliki Kanda na Waamini kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya jimbo la Shinyanga.
Misa hiyo ya kilele imetanguliwa na kongamano maaluum la mafundisho ya kiimani yaliyobeba mada mbalimbali pamoja na maombezi kwa watu wenye shida, ambalo limefanyika kwa muda wa wiki nzima katika uwanja wa kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo (mwenye miwani) kwa kushirikiana na Mapadre wengine akiongoza adhimisho la Misa takatifu ya kilele cha Jubilei ya miaka 25 ya Karismatiki Katoliki Jimbo la ShinyangaParoko msaidizi wa Parokia ya Lubaga Padre Paul Mahona akisoma somo la Injili kwenye MisaMisa inaendeleaPadre Peter Bahati wa shirika la Rozimini kutoka Jimbo la Tanga akitoa mahubiri kwenye Misa ya kilelel cha JubileiMkurugenzi wa utume wa Walei Jimbo Padre Josephat Mahalu akiwawekea mikono Karismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga mara baada ya kurudia viapo vya utume wao ndani ya KanisaMkurugenzi wa utume wa Walei Jimbo Padre Josephat Mahalu na Padre Peter Bahati wakiwawekea mikono Karismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga mara baada ya kurudia viapo vya utume wao ndani ya KanisaParoko wa Parokia ya Shinyanga mjini na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo Padre Anatoly Salawa akiwawekea mikono Karismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga mara baada ya kurudia viapo vya utume wao ndani ya KanisaPadre Kisumo akiwakomunisha baadhi ya waliohudhuria Misa ya Kilele cha JubileiParoko wa Parokia ya Mwadui Padre Michael Msabila akiwakomunisha baadhi ya waliohudhuria Misa ya Kilele cha JubileiPadre Anatoly Salawa akiwakomushi waaminiPadre Kisumo akipokea na kubariki Matoleokwenye MisaKarismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga wakiwa mbele ya Kanisa kwa ajili ya kurudia viapo vyaoPadre Kisumo akiwaongoza Karismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga kurudia viapo vyao vya utume ndani ya KanisaMapadre walioshiriki Misa ya Jubilei ya kilele cha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Karismatiki Jimbo la Shinyanga, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo na Paroko wa Parokia ya Shinyanga Mjini Padre Anatoly Salawa, wa pili ni Mkurugenzi wa utume wa Walei jimbo na Paroko wa Parokia ya Busanda Padre Josephat Mahalu, wa tatu ni Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo, wa nne ni Padre Peter Bahati wa Shirika la Rozimini kutoka Jimbo la Tanga na wa Mwisho ni Paroko wa Parokia ya Mwadui Padre Michael MsabilaWanakarismatiki Katoliki Jimbo la Shinyanga wakirudia viapo vyaoWanakwaya wa Karismatiki Katoliki wakiwa katika adhimisho la MisaMratibu wa Karismatiki Jimbo la Shinyanga Bw.William Chami akitambulisha wageni na kuwakaribisha Wanakarismatiki kwa ajili ya kurudia viapo vyaoMapadre walioshiriki Misa wakiwa katika Picha ya pamoja na makundi mbalimbali ya Wakarismatiki Jimbo la ShinyangaMapadre wakiwa katika Picha ya pamoja na watawa waliohudhuria Misa ya Jubilei ya Karismatiki
Post a Comment