" KIJANA MAJALIWA NI MZALENDO WA KWELI,RAIS SAMIA ATAKA APELEKWE JESHINI

KIJANA MAJALIWA NI MZALENDO WA KWELI,RAIS SAMIA ATAKA APELEKWE JESHINI

 


Na Fabius Clavery Misalaba Blog- Kagera.

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Kassim Mjaliwa ametoa maelekezo kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kumtafutia kazi jeshini  katika vikosi vya uokoaji kijana Jackson Majaliwa kufuatia ushujaa aliouonyesha  kwa kutenda uokozi kwa wasafiri 24 kati ya 43 waliopata ajali ya ndege iliyotokea November 06,2022 mjini Bukoba mkoani Kagera ikiwa ni shukrani za serikali kwa kijana huyo.

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maelfu ya waombolezaji, baada ya ibada ya kuaga miili 19 ya  marehemu wa ajali hiyo katika uwanja wa kaitaba,amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe.Samia Suluhu Hassan amempongeza  kijana huyo kwa uzalendo wake na ushujaa wa kuokoa  watu 24 ambao ni abiria wa ndege hiyo.

"Mh Rais ametupigia simu hapa na kwamba lile tendo alilofanya kijana huyu aliyeona ndege ile ikitua pale akiwa wakwanza na akaamua kwenda pale na kuufungua ule mlango kwa ujasiri wake huo,mweshimiwa Rais ameagiza akabidhiwe kwa waziri wamambo ya ndani naye pia atafutiwe nafasi kwenye jeshi la uokozi ili kijana huyu apate mafunzo zaidi ya ujasiri wake huo aingie kwenye jeshi hilo linalohitaji ujasiri kama aliouonyesha " ametangaza waziri mkuu Majaliwa

"mimi kama mtendaji mkuu naendelwa kumsisitiza waziri wa mambo ya ndani baada ya tukio hili akutane na kijana apate taratibu zake achukue anuani zake na kushuhudia akienda kwenye jeshi la uokozi mara moja,nichukie nafasi hii kumshukuru sana mh.Rais kwa maelekezo yake na ni mhakikishie kwamba maelekezo hayo tutayasimamia kwa ukaribu" ameongeza waziri mkuu

Kadhali kawaziri mkuu amewataka wananchi na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati ambao timu  wataalamu likiendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo mpaka hapo timu hii itakapo kamilisha uchunguzi na kutoa taarifa.

Kijana Jackson Majaliwa jmri wa miaka 20 pekee na amesema kuwa ameishia kidato chapili na mpaka sasa alikuwa anajiusisha na shughuli za uuzaji wa dagaa wabichi,kuhusu tamko la Rais ameeleza kufurahishwa nalo na kuishukuru serikali.

" agizo  la waziri mkuu nimelipokea vizuri,kwasababu hata mimi ilikuwa sehemu ya ndoto yangu na mimi nifanye kitu kwa ajali ya Taifa" Ameeleza kijana Majaliwa Jackson

Kwa upande wake waziri wa uchukuzi nchini prof.Makame Mbarawa amewatoa ofu wananchi ambapo amesema kuwa usafiri wa anga  ndio usafiri salama zaidi ulimwenguni hivyo ajali iliyotokea ni kutokana na hali mbaya ya hewa na sio matukio ya mara kwa mara.

Prof.Mbarawa ameongeza kuwa uwanja wa ndege wa Bukoba ni salama na utaendelea kutumika.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Kagera mh Albert Chalamila ameiomba serikali kupitia mfuko wa maafa kuwezesha mafunzo ya uokoaji kwa wananachi waishio karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba ambao ndio walishiriki pakubwa kufanya uokozi baada ya ajali hiyo kutokea.

Ajali ya ndege hiyo imehusisha ndege ya kampuni ya Presicion Air iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Dar es salaam - Bukoba- Mwanza iliyokuwainaongozwa na Rubani Buruhani Rubanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post