Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema leo ameongoza shughuli ya kuaga miili ya watoto
watatu wasioona waliofariki kufuatia ajali ya moto ulioteketeza bweni katika shule
ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga na kusababisha vifo vyao.
Shughuli
ya kuaga miili ya watoto hao imefanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini , wa serikali, viongozi
wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na wananchi.
Akizungumza
kwenye shuguli hilo RC Mjema ameendelea kutoa pole kwa familia zilizopatwa na
msiba ambapo amesema kuwa serikali inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo
cha moto huo.
“Kwanza kabisa naomba
nitoe pole nyingi sana kwa familia kwa kupotelewa na watoto wetu hawa ambao
tulikuwa tunawategemea sana katika maisha kuona kwamba badae watakuja kuwa watu
wambao watasaidia familia lakini yote ni mipango ya Mungu tuipokee kwahiyo tunaomba
tutoe pole nyingi sana”
“Jambo hilo limefanyika
serikali bado inaendelea kufanya kazi yake ya kuweza kubaini chanzo
kilichotokea ni nini ili jambo hili liziweza kutokea tena hasa katika maeneo ya
watoto wetu wanaoishi kwenye mabweni”.amesema RC Mjema
Akizungumza
kwa niamba ya chama cha mapinduzi CCM Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya wa Shinyanga vijijini Bwana Edward Ngelela wakati akitoa pole amesema
katika kipindi hiki kila mmoja anapaswa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.
Usiku
wa kuamkia jana Novemba 23,2022 bweni wanalolala wanafunzi wa kike wenye
ulemavu liliungua moto na kusababisha vifo vya watoto watatu ambao miili yao
imeagwa leo kiserikali.
Waliofariki
Dunia ni Miirium Limbu ambaye mwili wake umesafirishwa kwenda Wilayani Kishapu
mahali alipozaliwa, Catherine Paulo mwenye mika 10 ambaye mwili wake umesafirishwa
kwenda Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu na Caren Mayenga mwenye miaka 9 ambaye
amesafirishwa kwenda wilayani Itilima
Mkoani Simiyu.
Miili ya watoto hao ikibebwa kusafirishwa kila mtoto alikozaliwa.
Post a Comment