" SERIKALI YAAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MRADI WA REA SHINYANGA KUKAMILISHA KWA WAKATI

SERIKALI YAAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MRADI WA REA SHINYANGA KUKAMILISHA KWA WAKATI



Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Serikali Mkoani Shinyanga imewaagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa kusambaza umeme vijijini REA, kukamilisha kazi hiyo ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Joseph Mkude kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa REA kilichofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkude amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wanakuwa kwenye maeneo ya utekelezaji wa mradi kama ilivyoelekezwa na Waziri wa nishati Januari Makamba, ikiwa ni pamoja na kutoa ripoti ya utendaji kazi kwa wakati.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa miradi ya jamii kama vile umeme ameweka kipaumbele kufikisha umeme hadi vijijini na hadi kwenye vitongoji ametafuta fedha ikapatikana na fedha haitumiki kutokana na changamoto zetu zinazotokana na sisi wenyewe”.

“Lakini pia nimshukuru waziri wa nishati Januari Makamba kwa kuongea na nyie wakandarasa na kuwapa muda ametoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwetu sisi tuseme tu leo tumekutana ni kikao cha kwenda kufanya kazi lakini tunaelekeza kuwa mnatoa taarifa kila baada ya wiki moja pamoja na ratiba yenu hiyo lakini kuwa saiti wakati wote wa utekelezaji ili kujua kama kunachangamoto yoyote ambayo mnakutana nayo ambayo itakwamisha utekelezaji wa miradi hii”.amesema Mkude

Msimamizi mkuu wa mradi huo unaotekelezwa katika wilaya za shinyanga na Kishapu, Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya umeme Suma JKT Meja James Mhame ameahidi kutekeleza mradi huo kwa wakati kama ilivyoagizwa na serikali.

“Tunapenda kuahidi kwamba kazi hii tunakwenda kuikamilisha kwa wakati kwa sababu vifaa muhimu ambavyo vinahitajika kukamilisha kazi hii kama nguzo, mita na transifoma tayari zimeshafika hapa Mkoani Shinyanga na tayari tumeshasimamia transifoma tatu ndani ya vijiji vitatu vya wilaya ya Kishapu lakini pia tumeshasimamia na kuvuta waya vijiji 16 ndani ya wilaya ya Kishapu na wilaya ya Shinyanga vijijini kwahiyo nimtoe wasiwasi mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwamba tunakwenda kukamilisha hii kazi kwa wakati na bila kuongeza muda”.amesema Meja Mhame

Kwa upande wake mkandarasi wa kampuni za Tontan project Technology mhandisi Revocatus Silivester ametaja hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo huku akiahidi kukamilisha kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba.

“Hadi sasa tumeshasimamisha nguzo na tumeshafikia vijiji 15 kwahiyo kabla yah ii wiki kuisha tutakuwa tumewasha vijiji kumi kwa sababu sasahivi tayari matirio tumeshapokea kwa asilimia 30 pia wiki ijayo tunapokea nguzo elfu nne kwahiyo mpango wetu kazi kwa mwezi wa pili na wa tatu tunahakikisha tunavifikia vijiji 56 hadi kufika mwezi was aba tutakuwa tumekamilisha vijiji 146”amesema Mhandisi Revocatus

Wakizungumza kwa niaba ya wabunge wa jimbo la Kahama na Kishapu wawakilishi katibu wa mbunge jimbo la Kahama Abdul Mpei na katibu wa mbunge jimbo la Kishapu Godfrey Mbussa wameonyesha kutorizishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Wamesema kuwa hadi sasa hakuna hatua zozote zilizofanyika katika utekelezaji wa mradi huo na kwamba malalamiko ni mengi kwa wananchi juu ya wakandarasa hao.


Post a Comment

Previous Post Next Post