" STENDI YA KAYANGA NA UWANJA WA MICHEZO WA BASHUNGWA KUONGEZA MAPATO YA NDANI HALMASHAURI YA KARAGWE.

STENDI YA KAYANGA NA UWANJA WA MICHEZO WA BASHUNGWA KUONGEZA MAPATO YA NDANI HALMASHAURI YA KARAGWE.



Na Fabius Clavery, Misalaba Blog


Mbunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amesema kukamilika kwa Stendi ya Mabasi ya Kayanga na Ujenzi wa uzio wa Uwanja Michezo wa Bashungwa vitachangia kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya Karagwe.


Bashungwa ameeleeza hayo Januari 29, 2023 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Stendi ya Mabasi Kayanga na Ujenzi wa Uzio wa uwanja wa Michezo wa Bashungwa uliopo katika mji wa Kayanga Wilaya Karagwe.


Bashungwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Karagwe kwa kutenga mapato ya ndani kuwezesha ujenzi wa stendi ya Mabasi ya Kayanga unaoendelea ambao unatekelezwa kwa awamu tofauti kwa ubia wa Serikali na Sekta binafsi.


Aidha, Bashungwa amesema Ujenzi wa stendi hiyo umeenda sambamba na ufungaji wa taa za usiku za barabarani katika mitaa ya mji wa kayanga na Omurushaka pamoja na maeneo baadhi ya Mji katika barabara kuu.


Kadhalika, Wakati akikagua Uwanja wa Michezo wa Bashungwa, ameeleza kuwa mradi huo utaisaidia halmshauri kuongeza mapato ya ndani kutokana na shughuli mbalimbali za kijamii na matamasha yatakayofanyika katika uwanja huo.


Bashungwa amesema ataendelea kutafuta wadau mbalimbali ambao watasaidia michango ya kuwezesha uwanja huo kujengewa uzio, ambapo pia utachangia kuinua Michezo na vipaji mbalimbali katika mkoa Kagera.


Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Bashungwa unatekelezwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri, Ofisi ya Mbunge na Michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.


Sambamba na hayo, Bashungwa amesema katika mwaka huu fedha 2022/23 kabla ya mwezi Juni Halmashauri wilaya Karagwe itapokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Karagwe ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Mbunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa akizungumza

Post a Comment

Previous Post Next Post