Wafanyabiashara na
wananchi wengine wanaotumia mnada wa Seke uliopo katika kata ya SekeBugoro
Wilayani kishapu Mkoani Shinyanga, wameitaka Halmashauri hiyo kujenga vyoo
katika eneo hilo, kama hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Wameiambia Misalaba
Blog kuwa kukosekana kwa huduma ya choo katika mnada huo inaweza kuchangia
magonjwa ya mlipuko kutokana na watu wanaofanya shughuli katika eneo hilo
kujisaidia ovyo.
Wameiomba halmashauri
hiyo kutatua changamoto hiyo kama hatua ya ya kuchukua tahadhari dhidi ya
magonjwa ya mlipuko, kwani tangu kuanza kwa mnada huo Mwaka 1984 hakuna huduma ya choo katika eneo hilo.
Wamesema wamekuwa
wakijisaidia ovyo hali inayotishia usalama wa afya zao, na kwamba licha ya kuwasilisha changamoto
hiyo kwenye mamlaka husika lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Halmashauri ya Kishapu
Dotto Yahaya amekiri kuwepo kwa
changamoto hiyo katika mnada wa
Seke ambapo ameeleza kuwa changamoto hiyo wamekuwa wakiiwasirisha kwa viongozi
mbalimbali akiwa mtendaji wa kata, afisa biashara wa Halmashauri hiyo ambao
wote hawakutekeleza ahadi zao.
“Hili
jambo nimelifuatilia sana alikuja mtendaji wa kata tukamwambia afisa biashara
wa Wilaya ya Kishapu bado ananipa ahadi lakini utekelezaji wake na ushirikiano
tu kwetu haupo kwahiyo tunaomba serikali ngazi ya juu kama ni mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga atusaidie tusije tukafika huko tunakoelekea”.
“Athari nyingi tu huwa zinatokea mimi
nashuhudia watu wengi wanasumbuliwa na tumbo kwa sababu ya utumiaji wa maji ya
kwenye madimbwi ya maji yanayozunguka mnada huu, watu huwa wanajisaidia haja
zao hovyo kwenye vichaka”.amesema
Mwenyekiti Yahaya
Naye katibu wa wafanyabiashara David Liwa ameeleza umuhimu wa vyoo katika mrada huo wa Seke uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.
“Swala
la choo tuliwaita wakaja tukaongea nao viongozi kutoka Halmashauri lakini mpaka
sasa hawatekelezi sisi tumechoka kujisaidia ovyo kama wanyama, sisi bado
hatujagoma kutoa ushuru lakini tunawapa muda tena endapo wakishindwa sisi
tutafanya maandamano ya amani kudai haki zetu maana kipindi cha nyuma tulitaka
kufanya mgomo wa kutoa ushuru
wakatuambia tukigoma wanakuja kufunga mnada huu”.amesema
Liwa
Mnada wa Seke uliopo
kijiji cha Ididi kata ya Bugoro Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
ambao pia unajumuisha Gulio la wiki unakadiriwa kuwa na takribani watu Mia tano
na kwamba hakuna vyoo katika eneo hilo hali inayoendelea kuathiri afya kwa
wafanyabishara na wananchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Halmashauri ya Kishapu Dotto Yahaya akielezea changamoto katika mnada huo.
katibu wa wafanyabiashara David Liwa akielezea changamoto zilizopo katika mnada huo.
Post a Comment