Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ameendelea kuwasihi wananchi kuacha vitendo
vya uhalifu na kwamba wanapaswa kushirikiana na jeshi hilo katika kutokomeza
uhalifu.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa
ya misako na doria zilizofanywa na jeshi hilo katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Disemba 20,
2022 hadi Januari 23,2023 amewasisitiza wananchi wa Mkoa wa Shinyanga
kushirikiana na jeshi hilo ili kutokomeza uhalifu.
Kamanda Magomi amewataka wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wahalifu badala ya kuwafikisha
katika vituo vya Polisi kwani kitendo hicho ni kosa la jinai na kinahatarisha
usalama wa raia.
Amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu 10 wanaotuhumiwa
kujihusisha na vitendo vya uhalifu
ikiwemo wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande
cha nne Tabora-Isaka na tayari wameshafikishwa mahakamani.
Ameeleza kuwa jeshi hilo
limejipanga kikamilifu kuhakikisha linadhibiti mianya yote ya vitendo vya wizi
katika mradi huo, ambapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu watakaobainika
kujihusisha na vitendo hivyo.
Wakati huo huo Kamanda
Magomi ametaja vitu na vielelezo mbalimbali vya wizi vilivyokamatwa kwa kipindi
cha Mwezi mmoja kupitia doria na misako hiyo ikiwemo nyara za serikali pamoja
na pikipiki zilizokuwa zinatumika kwa wizi.
“Tumefanikiwa
kukamata vitu na vielelezo mbalimbali kama ifuatavyo, jumla ya pikipiki 8
ambazo zilikuwa zinatumika kwa wizi au za wizi zilikamatwa, Bangi kilo kumi na
kete 278, tulikamata nyara za serikali ambazo ni mikia 21 ya Nyumbu, maganda 5
ya Mayai ya Mbuni, ngozi moja yap aka pori, kipande kimoja cha ngozi ya mbuzi
mawe, Miiba 44 ya Nungunungu , vipande vitatu vya mkonga wa tembo, Mikia mitatu
ya Ngiri, vipande vitatu vya magamba ya Kobe, kucha tano zap aka pori, kipande
kimoja cha jino la Tembo, kipande kimoja cha ngozi ya Fungo pamoja na kipande
kimoja cha pembe ya Korongo”.ametaja kamanda Magomi
“Vile
vile tuliweza kukamata Meter moja ya Tanesco, Solar panel moja, Control box
moja ya mtambo, Tv nne, Subwoofer moja, mafuta ya Petrol lita 225, bidhaa
mbalimbali za dukani, seti moja ya mziki wa disko, pombe kali za aina
mbalimbali, pombe ya moshi lita kumi, Computer moja, Godoro moja, viti 10 vya plastic,
nyaya za miundombinu ya mawasiliano ya TTCL, vyuma vya miundombinu ya barabara,
madumu 42 yaliyotaka kutumika katika wizi wa mafuta huko maeneo ya Seke pamoja
na Battery mbili kubwa za gari”.amesema kamanda Magomi
“Lakini
pia jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga tuliokota pokipiki 9 ambazo kwa namna
moja ama nyingine zilisahaulika au kutupwa katika maeneo mbalimbali kutokana na
sababu tofauti ikiwa ni pamoja na uhalifu na ulevi”.
“Kesi
moja ya kubaka ilihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi moja ya ukatili wa motto
ilihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, kesi moja ya ushirikiana ilihukumiwa
kifungo cha nje miezi sita, kesi moja ya uvunjaji ilihukumiwa kifungo cha miezi
sita jela pamoja na kesi mbili za kupatikana na Bangi zilihukumiwa kifungo cha
miezi sita jela”.amesema Magomi
Katika hatua nyingine
Kamanda Magomi amekemea watu wanaojihusisha na lamri chonganishi ambazo
zimetajwa kuwa chanzo cha vitendo vya ukatili katika jamii.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Post a Comment