" HALMASHAURI ZA MKOANI RUKWA ZAAGIZWA KUTUMIA SHERIA NDOGONDOGO ILI KUREJESHA UOTO WA ASILI.

HALMASHAURI ZA MKOANI RUKWA ZAAGIZWA KUTUMIA SHERIA NDOGONDOGO ILI KUREJESHA UOTO WA ASILI.








NA: FRANCO NKYANDWALE. RUKWA.




MKuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ametoa agizo kwa Maafisa Tarafa na Kata kusimamia na kuhamasisha wananchi upandaji wa miti kwenye maeneo yao ili kutunza mazingira.




Katika kuhakikisha kampeni ya urejeshaji uoto wa asili mkoani Rukwa unafanikiwa, hivyo Sendiga, amezitaka Halmashauri za Nkasi, Sumbawanga Manispaa, Sumbawanga DC, na Kalambo kuboresha sheria ndogo ndogo ili waweze kuchua hatua kwa waharibifu wa mazingira.






Kwa mujibu wa taarifa ya leo ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Desemba 2022 hadi Januari 2023, jumla ya miche 250,190 imepandwa kati ya lengo la miti 1,500,000.

Post a Comment

Previous Post Next Post