Zaidi ya Ekari 72 za Mazao Pamoja na Nyumba 14 za Wakazi katika kijiji cha Image kilichopo kata ya Kidegembye halmashauri ya wilaya ya Njombe Mkoani Njombe zimeharibiwa Vibaya kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha hapo Februari 6 Mwaka huu na Kusababisha baadhi ya Wakazi katika Kijiji Hicho Kukosa hifadhi.
Baada ya kutokea Maafa hayo Serikali ya Wilaya ya Njombe pamoja na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Lupembe imefika Katika kijiji hicho na kujionea namna maafa yalivyojitokeza ambapo kwa niaba ya Serikali Katibu tawala Wilaya ya Njombe Emanuel George licha ya kutoa pole amewataka wananchi Kuondoa miti mikubwa iliyopo karibu na Makazi.
Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe.Edwin Enosy Swalle Katibu wa Mbunge huyo Israel Mhada amekabidhi bati 100 kwa ajili ya kuasidia Wananchi waliokutwa na Madhira hayo.
Ibrahimu Fungo ni Afisa Kilimo kutoka Halmashauri wa Wilaya ya Njombe ambaye amewataka Wananchi wa kijiji hicho walioathiriwa na Mvua hizo kuanza kupanda mazao ya muda mfupi huku akiwaasa kuhifadhi chakula walichonacho.
Kufuatia Maafa hayo Wananchi wa kijiji hicho akiwemo Rose Stefan, Lameck Mhada na Debio Kuchungula wamesema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na maafa hayo kwani wamekosa hata makazi na kulazimika kuomba hifadhi kwa majirani.
Imeelezwa Kuwa Mvua Hiyo Iliyonyesha Hapo Feburuary 6 Mwaka Huu Iliambatana na Mawe Mengi ambayo baadhi ya Maeneo hadi Hivi sasa hayajayeyuka.









Post a Comment