" POLISI IRINGA WANASA WEZI WA MAFUTA AKIWEMO MCHINA WA WA NYARA ZA SERIKALI

POLISI IRINGA WANASA WEZI WA MAFUTA AKIWEMO MCHINA WA WA NYARA ZA SERIKALI




Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionesha Kobe mmoja kati ya watano waliokamatwa Kwa raia wa China
.....................................




JESHI la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia meneja wa kampuni ya CRJE Zack Zhang (33)Raia wa China Kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni Kobe .


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)Allan Bukumbi aliwaeleza waandishi wa Habari Leo kuwa tukio hilo lilitokea February 7 majira ya Saa 8 mchana Kijiji Cha Mbugani kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa.




Alisema askari wakiwa Katika doria walimkamata mchina huyo akiwa amefuga Kobe watano wakiwa kwenye kasha la mbao ndani ya Kambi Yao ya CRJE inayojishughulisha na utengenezaji wa mifereji ya maji kwenye skimu ya umwagiliaji bila kuwa na kibali chochote Cha maliasili baada ya kufanya upekuzi wa kutokana na taarifa fiche .


Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia Sasa kujibu tuhuma hizo .


Wakati huo huo jeshi la Polisi mkoani Iringa limewakamata wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji mafuta aina ya Dizeli na Petroli ambayo ni ya wizi .




Kamanda Bukumbi alisema katika oparesheni iliyofanyika kuanzia Januari 29 Hadi February 5 mwaka huu wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa walifanikiwa kukamata matuhumiwa mbali mbali wa wizi wa mafuta .


Alisema waliokamatwa ni Daud Mbumila (57) mkazi wa Frelimo Majengo mapya Mjini Iringa ambaye ni dereva aliyekutwa ameegesha porini Lori lenye namba za usajili T 123 BFB aina ya Scania (Tank ) na watuhumiwa wengine 17 wakiwa na Vifaa vya ununuzi wa mafuta .




Alivitaja Vifaa walivyokamatwa navyo kuwa ni madumu 158 yakiwa na mafuta aina ya Dizel Lita 482 na madumu matupu 305 ,piki piki mbili aina ya Haojue na Fekon ambazo zilikuwa zokitumika kusafirisha mafuta hayo ,mipira 21 ya kunyonyea mafuta kwenye Malori ,mapipa nane na chujio sita .



Kuwa wizi huo wa mafuta umefanyika kwenye Malori yanayofanya




Aidha Katika Oparesheni hiyo Polisi waimkamata Shabibu Mbosa (20) mkulima mkazi wa Mtaa wa kaguo Kata ya Makorongoni mjini Iringa na Epiana Mwakalasa (28) fundi Umeme mkazi wa Chemchem wakiwa na bangi kete 104 baada ya kupekuliwa chumbani kwao alisema watuhumiwa hao walikuwa wakijihusisha na biashara ya bangi hizo .


Kamanda Bukumbi alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao na kutoa Rai Kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kufichua waharifu na uhalifu Katika maeneo yao .

Post a Comment

Previous Post Next Post