" WALIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU WATAKIWA KUTEKELEZA VIGEZO 19

WALIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU WATAKIWA KUTEKELEZA VIGEZO 19

Anaripoti Respice Swetu, Misalaba Blog

Kufuatia kutolewa kwa vigezo 19 vya kupima wa utendaji kazi wa walimu wa shule za msingi nchini, idara ya elimu awali na msingi katika halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imewataka walimu kuvitekeleza vigezo hivyo,
Maagizo hayo yametolewa kwa nyakati tofauti na maafisaelimu wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu walipokuwa wakikutana na walimu wa halmashauri hiyo kuweka mikakati ya kutekeleza vigezo hivyo.

Walisema kuwa, vigezo hivyo ni muhimu kwa kuwa vitasaidia kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kitaifa pamoja na kuiwezesha halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ambayo hayakuwa mazuri.

Akitoa taarifa ya matokeo ya mitihani hiyo, afisaelimu taaluma wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph Maiga alisema halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imekuwa ya tano kati ya halmashauri nane za mkoa wa Kigoma kwenye mtihani wa kuhitimu darasa la saba na ya saba katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne.

"Matokeo haya sio mazuri kwetu na hayakuwa mazuri hata kitaifa na kutokana na hali hiyo, Ofisi ya Rais Tamisemi na wizara ya elimu wamefanya tathmini na kuja na vigezo 19 vya upimaji vitakavyosaidia kupandisha ufaulu huo", amesema.

Akivitaja vigezo hivyo Maiga alisema kuwa miongoni mwa vigezo vilivyopo ni kwa kila shule kufanya tathmini pindi matokeo ya mitihani yanapotoka, kudhibiti utoro shuleni na kukabiliana na mdondoko wa wanafunzi.

Aliendelea kueleza kuwa, kigezo kingine ni walimu kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba kwa asilimia 95 huku wanafunzi wa darasa la nne wakitakiwa kufaulu kwa asilimia 100.

Aidha vigezo hivyo vinaitaka kila shule kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha watoto wa darasa la kwanza wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Vigezo hivyo vilivyotolewa kwa nchi nzima, vinawataka pia walimu kuwafundisha watoto wa darasa la tatu stadi za somo la Kiingereza kwa ukamilifu.

Akifafanua kuhusu stadi hizo, Maiga alizitaja kuwa ni za kusoma, kuandika, kuhesabu na kusikiliza.

Vigezo hivyo vimeutaja wajibu wa walimu kushirikiana na kamati za shule, wazazi na jamii ili kuwezesha upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni.
Akizungumza na walimu wa kata ya Nyamidaho katika kikao kilichofanyika kwenye shule ya Msingi Mvugwe, afisaelimu wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Elestina Chanafi amesema, ni jukumu la kila mmoja kutekeleza vigezo hivyo.

"Baada ya kuviwasilisha vigezo hivi tutaanza kupita kuona utekelezaji wake, tumepewa siku mbili tu za kukaa ofisini na siku zinazobaki tutakuwa shuleni", amesema.

Kupitia kikao hicho, Chanafi amewataka walimu kuifanya kazi yao kwa kujituma, kujiendeleza na kuwa wabunifu.

"Mnatakiwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu na kuacha alama katika shule zenu, msichanganye muda wa kazi na mambo mengine na anayeona biashara inalipa kuliko kazi aache kazi", amesema.

Katika hali inayoonesha kuweka msisitizo kwenye utekelezaji wa vigezo hivyo, kwa mara nyingine Chanafi aliwaambia walimu hao kuwa mwaka huu afe kipa afe beki akimaanisha dhamira aliyonayo ya kuinua taaluma.
Kauli hiyo aliitoa pia kwenye kikao kama hicho alipokuwa akiongea na wadau wa kata ya Buhoro hivi karibuni.

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imekamilisha mzunguko wa maafisaelimu kukutana na walimu pamoja na wadau wengine kuweka mikakati ya utekelezaji wa vigezo hivyo ambapo takribani walimu 800 wa shule 85 za msingi, wamefikiwa sambamba na viongozi wa kamati za shule, wawakilishi wa madhehebu ya dini, watendaji wa vijiji na watendaji wa kata.

Baadhi ya walimu na wadau wengine (pichani) wakipokea maelekezo ya utekelezaji wa vigezo vya kupima utendaji kazi.
Walisema kuwa, vigezo hivyo ni muhimu kwa kuwa vitasaidia kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kitaifa pamoja na kuiwezesha halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa upimaji wa darasa la nne na wa kuhitimu darasa la saba.

Akitoa taarifa ya matokeo ya mitihani hiyo iliyofanyika mwaka jana, afisaelimu taaluma wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph Maiga alisema halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imekuwa ya tano kati ya halmashauri nane za mkoa wa Kigoma kwenye mtihani wa kuhitimu darasa la saba na ya saba katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne.

"Matokeo haya sio mazuri kwetu na hayakuwa mazuri hata kitaifa na kutokana na sababu hiyo, Ofisi ya Rais Tamisemi na wizara ya elimu wamefanya tathmini na kuja na vigezo 19 vya kupima utendakazi vitakavyosaidia kupandisha ufaulu huo", amesema.

Akivitaja vigezo hivyo Maiga alisema kuwa miongoni mwa vigezo vilivyopo ni kwa kila shule kufanya tathmini pindi matokeo ya mitihani yanapotoka, kudhibiti utoro shuleni na kukabiliana na mdondoko wa wanafunzi.

Aliendelea kueleza kuwa, kigezo kingine ni walimu kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba kwa asilimia 95 huku wanafunzi wa darasa la nne wakitakiwa kufaulu kwa asilimia 100.

Aidha vigezo hivyo vinaitaka kila shule kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha watoto wa darasa la kwanza wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Vigezo hivyo vilivyotolewa kwa nchi nzima, vinawataka pia walimu kuwafundisha watoto wa darasa la tatu stadi za somo la Kiingereza kwa ukamilifu.

Akifafanua kuhusu stadi hizo, Maiga alizitaja kuwa ni za kusoma, kuandika, kuhesabu na kusikiliza.

Vigezo hivyo vimeutaja wajibu wa walimu kushirikiana na kamati za shule, wazazi na jamii ili kuwezesha upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni.

Akizungumza na walimu wa kata ya Nyamidaho katika kikao kilichofanyika kwenye shule ya Msingi Mvugwe, afisaelimu wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Elestina Chanafi amesema, ni jukumu la kila mmoja kutekeleza vigezo hivyo.

"Baada ya kumaliza kuviwasilisha vigezo hivi tutaanza kupita ili kuona utekelezaji wake, tumepewa siku mbili tu za kukaa ofisini na siku zinazobaki tutakuwa shuleni", amesema.

Kupitia kikao hicho, Chanafi amewataka walimu kuifanya kazi yao kwa kujituma na kuwa wabunifu.

"Mnatakiwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu na kuacha alama katika shule zenu, msichanganye muda wa kazi na mambo mengine na anayeona biashara inalipa kuliko kazi aache kazi", amesema.

Katika hali inayoonesha kuweka msisitizo kwenye utekelezaji wa vigezo hivyo, kwa mara nyingine Chanafi aliwaambia walimu hao kuwa mwaka huu afe kipa afe beki akimaanisha dhamira aliyonayo ya kuinua taaluma.
Kauli hiyo aliitoa pia kwenye kikao kama hicho alipokuwa akiongea na wadau wa kata ya Buhoro hivi karibuni.

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imekamilisha mzunguko wa maafisaelimu kukutana na walimu pamoja na wadau wengine kuweka mikakati ya utekelezaji wa vigezo hivyo ambapo takribani walimu 800 wa shule 85 za msingi, wamefikiwa sambamba na viongozi wa kamati za shule, wawakilishi wa madhehebu ya dini, watendaji wa vijiji na wa kata.

Post a Comment

Previous Post Next Post