" PADRE KIZITO AWAKUMBUSHA WAAMINI KUENDELEA KUWATIA MOYO NA KUWAOMBEA WATAWA

PADRE KIZITO AWAKUMBUSHA WAAMINI KUENDELEA KUWATIA MOYO NA KUWAOMBEA WATAWA

 

Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Kizito Nyanga, amewasihi waamini kuendelea kuwaombea watawa , ili waendelee kustahimili katika maisha waliyoyachagua ya kujitoa bila kujibakiza, kwa ajili ya kumtumikia Mungu na Kanisa.

Padre Kizito ametoa wito huo wakati akiongoza Misa takatifu ya maadhimisho ya siku ya Watawa, iliyofanyika kijimbo leo Jumamosi tarehe 04.02.2023, katika Kanisa la Mtakatifu Bikra Maria Mediatrix Parokia ya Buhangija mjini Shinyanga.

Amewaelezea WATAWA kuwa ni watu ambao wamejiweka wakfu kwa  Mungu kupitia nadhiri za useja, ufukara na utiifu, ili kupata nafasi nzuri ya kumtumikia Mungu pasipo kikwazo cha Mume au Mke, wakifuata maandiko matakatifu kupitia waraka wa kwanza wa mtume Paul kwa Wakorinto unaosema kuwa “Bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.Yeye asiyeolewa hujishusha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho 1kor 7:33-34”

Amewapongeza WATAWA wote kwa jinsi ambavyo wanafanya bidii kumhubiri Kristo kupitia karama na huduma mbalimbali za jamii wanazozifanya katika mazingira yote ikiwemo ya Jimbo la Shinyanga lenye changamoto nyingi za kijamii.

Padre Kizito amebainisha kuwa, watawa wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali za kimazingira na kijamii ikiwemo mtazamo hasi  katika macho ya kidunia  kwamba, jambo la kuishi bila kuoa au kuolewa haliwezekani na kusababisha wadharauliwe na baadhi ya watu, lakini wameweza kuishi na kuyafurahia maisha hayo kutokana na neema ambazo mwenyezi Mungu anawajalia.

Amewasihi waamini Wakatoliki kuwatia kwa kuyachagua maisha hayo, pamoja na kuendelea kuwaombea ili Mungu awatie nguvu  na wawe na umoja katika utume wao.

Padre Kizito ambaye ameongoza Misa hiyo ya maadhimisho ya siku ya Watawa kwa niaba ya Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ametumia nafasi hiyo pia kumpongeza Sister Regina Muzi wa shirika la Mtakatifu Maria Malkia wa Afrika ambaye ametimiza miaka 50 ya utawa.

Sister Muzi ambaye anafanya utume wake katika Jimbo la Shinyanga, ameungana na watawa wenzake wawili wa shirika hilo ambao ni Sister  Regina Lwimo na Sister  Mary Dolorosa wanaoadhimisha miaka 25 ya utawa, mwaka huu 2023.

Maandamano ya Watawa wakiwa wametanguliwa na walelewa wa shirika la jimbo la Shinyanga la Mt.Bikra Maria Mama wa Huruma kuelekea Kanisani kwa ajili ya adhimisho la Misa Takatifu
Wanakwaya wa Kwaya ya Watakatifu Petro na Paul Mitume Parokia ya Buhangija wakiwa katika maandamano kujelekea Kanisani
Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga akibariki maji ya baraka ambayo yatatumika kubariki mishumaa ambayo wamewasha watawa ikiwa ni ishara ya mwanga wa Kristo
Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga akitoa neno la utangulzi wa Misa takatifu ya maadhimisho ya siku ya Watawa
Watawa, walelewa na baadhi ya waamini wakiwa katika adhmisho la Misa takatifu
Somo la kwanza likisomwa na mmoja wa walelewa wa shirika la kijimbo.
Somo la pili likisomwa na mmoja wa walelewa wa shirika la jimbo
Padre Felix Wagi wa shirika la Mapadre Waselesiani wa shirika la Mt. Don Bosco ambaye pia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco- Didia akisoma somo la Injili
Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga akitoa homilia

Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga akipokea matoleo
Adhimisho la Misa takatifu likiendelea kwa ushiriki wa Mapadre wote waliohudhuria Misa hiyo
Mkurugenzi wa utume wa walei Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Josephat Mahalu akiwa katika adhimisho la Misa takatifu
Adhmisho takatifu la Misa likiendelea, kushoto kwa Makamu wa Askofu ni Padre Paul Kitali ambaye ni Mlezi wa Watawa Jimbo la Shinyanga
Padre Felix akiwakomunishwa Watawa
Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga (katikati) akiwa Kanisani, kushoto ni Mlezi wa Watawa Jimbo Padre Paul Kitali wa shirika la damu azizi ya Yesu ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Old Maswa na kulia ni Padre Felix Wagi wa Shirika la Mt.Don Bosco ambaye pia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco-Didia
Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo (kushoto) akiwa katika adhimisho la Misa ya Watawa, katikati ni Paroko wa Parokia ya KItangili Padre Baltazar Zengo na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa utume wa Walei Jimbo na paroko wa Parokia ya Busanda Padre Josephat Mahalu
Mwenyekiti wa umoja wa watawa Jimbo la Shinyanga Brother Francisco Bega wa Shirika la Brothers of Charity akizungumza kwa niaba ya Watawa mara baada ya Misa
Mlezi wa watawa Jimbo Padre Paul Kitali akitoa neno la shukrani na kuwatambulisha Mapadre ambao wameshiriki adhimisho la Misa takatifu
Makamu wa Askofu Padre Kizito Nyanga akiwa katika picha ya pmaoja na Masister wa shirika la Mtakatifu Mt. Maria Malkia wa Afrika ambao mwaka huu wanaadhimisha miaka 25 ya utawa, kushoto ni Sister Regina Lwimo na kulia ni Sister Mary Dolorosa mara baada ya Misa

Post a Comment

Previous Post Next Post