
Baba Mtakatifu Farancisco, amemteua Askofu Mkuu PROTACE RUGAMBWA, kuwa Askofu Mkuu mrithi wa Jimbo kuu la Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Charles Kitima, uteuzi huo umefanyika leo tarehe 13.04.2023.
Kabla ya uteuzi huo, Askofu Mkuu Rugambwa alikuwa katibu Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji wa watu mjini Vatican.
Askofu mkuu Protas Rugambwa, alizaliwa mnamo Mei 31 mwaka 1960, huko Bunena, Jimbo Katoliki la Bukoba. Baada ya kumaliza elimu yake ya Msingi alijiunga na elimu ya Sekondari katika Seminari ndogo za Katoke Rulenge na Itaga Tabora kwa masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita.Alijiunga na masomo ya Falsafa katika Seminari kuu ya Kibosho iliyoko Jimbo Katoliki la Moshi na akaendeleo na Masomo ya Thelojia katika Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga Segerea, iliyopo Jimbo kuu la Dar es salaam.
Mnamo mwaka 2002 hadi 2008, aliombwa kwenda kusaidia kutoa huduma za kichungaji kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, utume ambao aliufanya kwa ufanisi mkubwa ambapo tarehe 18 Januari 2008, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akamteua kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na kuwekwa wakfu tarehe 13 Aprili 2008.
Post a Comment